Paul Kagame: Ukiona wenye mali wanageuka kuwa ombaomba ujue akili zao haziko sawa

Paul Kagame: Ukiona wenye mali wanageuka kuwa ombaomba ujue akili zao haziko sawa

If the owners of the natural resources go around begging, then you should know there's something wrong with their minds” - President Paul Kagame

My Take
Mdomo Kila mtu anao,swali Je yeye amefanya kipi Cha maana hapo Rwanda wakati Nchi yake ni LDC?


View: https://twitter.com/zoomafrika1/status/1751687168903246141?t=NxJF88fOVWuRygoaV1uIoQ&s=19

Zimbabwe na Kenya wameenda Italy kuomba 😆😆

View: https://twitter.com/ali_naka/status/1751742802591981687?t=nyIy2JtjceUcDTKN3AKIKw&s=19

Wenye PhD za kutembeza bakuli, ujumbe huu unawahusu.
 
Wakimbizi waliopo nchini mwetu ndio wezi wakubwa na wahujumu wa hili taifa
 
Mabasha zake si wanatumia vibaraka akiwemo yeye kuvuruga Congo!!?
Hivi chuki za Waisilamu wa Tanzania dhidi ya Paulo Kagame zinatokana na nin?
Au ni kwasababu ana Pua ya Kiarabu na yeye sio Muisilamu?
 
Baada ya Vikosi vya SADC kutua DRC ataongea mengi sana.
 
Moja ya Nchi zinazoongoza kupewa mosaada hapa Afrika ni Rwanda.

Hana hiyo jeuri ila mdomo anao.

Sawa. ila mdomo unasema ukweli.

Yaani ukubwa na utajiri wa Mkoa wa Geita tu unaizidi Rwanda yote .... Unlike na Rwanda sisi tuna mali nyingi sana.Halafu ni nchi ya AMANI (kama wanavyodai CCM) kwa miaka 62 lakini hamna la maana zaidi ya kuombaomba.
 
Sawa. ila mdomo unasema ukweli.

Yaani ukubwa na utajiri wa Mkoa wa Geita tu unaizidi Rwanda yote .... Unlike na Rwanda sisi tuna mali nyingi sana.Halafu ni nchi ya AMANI (kama wanavyodai CCM) kwa miaka 62 lakini hamna la maana zaidi ya kuombaomba.
Wadogo wenzie kina Equatorial Guinea au Cape Verde ni matajiri yeye anapiga mdomo wakati anapakana na Nchi Tajiri,ana Hifadhi za Wanyama,ana population kubwa na ana Madini.

Huoni huyo ni mjinga mmja ambae anatafuta excuses Kwa wajinga kama wewe?
 
Hata kama na yeye Rais wa Rwanda anaomba, bado kauli yake inaukweli tupu, na bahati mbaya hakutaja moja kwa moja ni nchi ipi hiyo!

Nchi ambazo tunazo Mungu ametupatia rasilimali nyingi mfano wa nchi za ulaya na saa nyingine tunazipita kwa uwingi wa rasilimali, lakini ndo tunazioomba mpaka inaonekana kana kwamba tunajiuza yaani

Ni uwongo kwamba tunaomba omba?

Ni uwongo kwamba sisi ni matajiri wa rasilimali kuzizidi hadi nchi za huko ng'ambo?

Shida yetu ni kukasirika tu pindi tukiambiwa ukweli badala ya kile kilichosemwa tukifanyie kazi ili tuondokane na aibu hizo,

Okay, fine, tufanye Kagame katukosea, basi tumnunie sasa tuone iwapo tutapata faida!

Tushughurisheni vichwa vyetu na tuwabariki wanaotwambia ukweli
 
Ni maneno fikirishi kwa wale watawala wanaozurura na bakuli kuomba.
"Akili ya mtu mweusi ina matatizo."- Profesa Robert Watson
 
Atulie mtu mwenye anatawala kamnchi kama wilaya moja tu hapa bongo na anatumia kila njia kulazimisha aonekane kichwa... ila siku sio nyingi ataaibika huyu.
Ni wilaya gani ukubwa wa Rwanda inaweza kujilinganisha na Rwanda?
 
Hivi chuki za Waisilamu wa Tanzania dhidi ya Paulo Kagame zinatokana na nin?
Au ni kwasababu ana Pua ya Kiarabu na yeye sio Muisilamu?
Utafiti wako umeonesha waislam wa tz wanamchukia kagame!?
 
Tunaposema huyu mtu anachuki na nchi yetu muwe mnaelewa na ana mapandikizi yake kibao kwenye mifumo yetu. Ni wakati Rais aifanyie kazi kikamilifu taarifa aliyopewa na CDF . Hilo dongo ni letu kabisa
Hili dongo linagusa almost nchi nyingi mno, iangalie Kenya, Uganda, Zimbabwe na nchi nyingi tu, sio kila kitu kikitamkwa ni cha kukichukia hapana, Yapo ambayo tunaambiana ili kuwekana sawa, turudi katika mstari sahihi, ni upumbavu kujenga biff kwa kauli ambazo zingine zina chembe za ukweli.
°HEKIMA ZA JINO LA MAMBA MZEE.
 
Back
Top Bottom