Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Twende taratibu ndugu yangu, kwa hiyo yeye ndio amekuwa msemaji wa Serikali au? Dkt. Abbass anafanya kazi gani?Wewe hujui kuwa Dsm ndio Tanzania?!
RC Dsm ni mkubwa kuliko Dr Abbas!Twende taratibu ndugu yangu, kwa hiyo yeye ndio amekuwa msemaji wa Serikali au? Dkt. Abbass anafanya kazi gani?
Dsm ni Dsm tu.
Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu!Ipo siku atamtangaza Magufuli kuwa ni mungu
Hizo machine zinakila kitu hadi dua zinasoma usiwe na shaka kijanaAjabu kivp mkuu,we hauna imani,?
Dr Malasusa ni kibaraka siku nyingi anafaidi matunda ya ukibaraka wake.Dr Malasusa wa KKKT, askofu Sosthenes wa Anglican, Kardinali Pengo wa Katotiki na shehe mkuu wa waislamu wote wa mkoa wa Dsm wamehudhuria mkutano huu wa kipekee!
Dr Abbas anaandika baruaTwende taratibu ndugu yangu, kwa hiyo yeye ndio amekuwa msemaji wa Serikali au? Dkt. Abbass anafanya kazi gani?
Dsm ni Dsm tu.
Mkui huwa huwezagi kabisa kujibu maswali..?RC Dsm ni mkubwa kuliko Dr Abbas!
maajabu ya Musa hivi Rais anajuwa kile kinafanyika au ndio ameamua kijana afanye yake.... Mungu tuepushe yajayo yanafurahisha. Kumpa Mamlaka kijana asie juwa wajibika niatari sana.Ni katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Karibu!
Kardinali Pengo na Sheikh wa mkoa kwa niaba ya Mufti wanauombea mkutano huo.
Sasa viongozi wa dini wanaangalia mkanda wa video unaomuonyesha RC Makonda akitolea ufafanuzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
------
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kasi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo inayofanywa na Rais wa Tanzania, John Magufuli inazidi maelekezo ya ilani ya CCM.
Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Novemba 18, 2019 katika mkutano wake na viongozi wa dini unaofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere (JNICC) ambako anawaeleza mambo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka minne.
Amesema kasi ya kiongozi mkuu huyo wa nchi ni kubwa kuliko ilani hiyo, kwamba amefanikiwa kwa kuwa amemtanguliza Mungu mbele.
Amesema uchapakazi huo ndio umewafanya watendaji wengine kumuiga.
“Kawafanya hata viongozi wa Serikali wanaotumia hirizi kumtaja Mungu kwanza. Mara nyingi ameweka wazi kuwa mambo yanavyokwenda kasi hata yeye mwenyewe anamshangaa Mungu,” amesema Makonda.
Amesema ameamua kukutana na viongozi wa dini ili kuwaeleza miradi inayotekelezwa katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Chanzo: Mwananchi