Paul Makonda akutana na Viongozi wa madhehebu na Taasisi za dini, asema anayoyafanya Rais Magufuli yanazidi maelekezo ya ilani ya CCM

Paul Makonda akutana na Viongozi wa madhehebu na Taasisi za dini, asema anayoyafanya Rais Magufuli yanazidi maelekezo ya ilani ya CCM

Ganda la mua la jana...
Usicho kithamini wewe, wenzako wanakitafuta.

Ila pia kiukweli watu humu wana wivu mpaka basi...

P
Pasco acha hizi mambo za kupiga bao

Ile ya Magu ulipenyezewa na watu wa kitengo

Hi utabuma.tu na utaibika mchana mweupe

Tutakuja kukumbusha Hapa 2025

Let's wait huna karama ya utabiri labda unampigia promo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam MuSa Salum amewataka viongozi wa dini kutoa azimio la kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo

Hayo ameyaeleza wakati wa mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini kwa ajili kuwaeleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeo tangu Rais Magufuli aingie madarakani.

Mi sijui hawa viongozi wa dini ni nini kimewapata? Eti “ mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini kwa ajili ya kuwaeleza utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo tangu Rais Magufuli aingie madarakani”

Swali je, hao viongozi wa dini wao hawaoni kwa macho yao au hawasikii kwa masikio yao hiyo miradi hadi waelekezwe na mkuu wa mkoa?
Au wao (viongozi) sio waelewa au ni wageni nchini?

Maswali ni mengi, ila itoshe tu kusema makundi yanaandaliwa mengi mno ya kusifu na kupamba hata visivyostahili. Ni majuzi tu bunge lilitoa azimio la kumuunga mkono mheshimiwa. Leo tena viongozi wa dini wametoa azimio hilo hilo. Mmmh [emoji15] haya!
 
Hapo Hakuna kiongozi wa dini hata mmoja hapo kuna wajasilia dini na wajasilia matumbo.
 
Listing ya viongozi was dini makanjanja
1. Pengo
2. Askofu wa TEC anaitwa Nyamwisobgo
3.Gamanya
4 shekhe wa Dar
5. Askofu Malasusa
6. Ongezea

Hawa hawataiona pepo,
Baba askofu Munga

Huyu nae mchunguzeni
 
Kwani sisi hatuna akili mpaka waanze kutushawishi sijui ujinga gani, hawa mashekhe wajinga wajinga wanaudharirisha uislamu
Wanaudhalilisha.

Sio wanaudharirisha.

Samahani madam.
 
Hata kijana wa sekondari hili angeweza kulieleza vizuri kuliko huyu anaye toa maelezo haya mbele ya Television huku kazungukwa na hao wajiitao watumishi wa Imani
Screenshot_20191118-230014.jpeg
 
Alafu Pengo akachekelea na kupiga vigelegele [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ni kwa vile maandiko yanatukataza kuwahukumu au kuwasemea hovyo watumishi wa Mungu, na sisi hatuna hakika hawa ni watumishi wa Mungu au wa CCM hivyo ngoja tunyamaze yeye mwenyewe atufunulie jibu sahihi. Lakini wanatukwaza sana
 
Alafu Pengo akachekelea na kupiga vigelegele [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nadhani Pengo kuna jambo alimkosea Mungu , kama kapigwa laana ili adhalilike
Naona tatizo la Makonda mmehamishia kwa Pengo.
Mlidhani tatizo lenu Pengo wakati wa WARAKA wa viongozi wa dini, mkamtusi na kumshambulia sana.
Mzee kastahafu sasa kaja mwingine Jimbo Kuu la DSM, na huko TEC kaja mwigine nae hafanyi kile mnachotaka.

Tatizo mnahukumu na kuwaza vitu kijujuu ndio maana hamjui mkadhibiti wapi panapo wakwamisha.

Tatizo lenu sio Pengo au Kanisa lolote, bali ni mikakati yenu ya kisiasa haiko mizuri, gia angani imewaondoa vichwa wengi sana upande wa mabadiliko ya kweli.
 
Makonda ni tatizo, anatakiwa awe msikilizaji na mtekelezaji kuliko kukimbilia vipaza sauti na majukwaa.
Hana umakini na kipaji cha kumudu vitu hivyo bila kufanya makosa.

Ajifunze kusikiliza zaidi na sio kuongea zaidi.
 
Naona tatizo la Makonda mmehamishia kwa Pengo.
Mlidhani tatizo lenu Pengo wakati wa WARAKA wa viongozi wa dini, mkamtusi na kumshambulia sana.
Mzee kastahafu sasa kaja mwingine Jimbo Kuu la DSM, na huko TEC kaja mwigine nae hafanyi kile mnachotaka.

Tatizo mnahukumu na kuwaza vitu kijujuu ndio maana hamjui mkadhibiti wapi panapo wakwamisha.

Tatizo lenu sio Pengo au Kanisa lolote, bali ni mikakati yenu ya kisiasa haiko mizuri, gia angani imewaondoa vichwa wengi sana upande wa mabadiliko ya kweli.
Gia ya angani ndiyo imesabababisha mkawaita watendaji ikulu na kuwaagiza waharibu form za wapinzani??
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimecheeeka....najaribu kuelewa hizo namba [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Gia ya angani ndiyo imesabababisha mkawaita watendaji ikulu na kuwaagiza waharibu form za wapinzani??
Mimi sio CCM, na nimekuwa muwazi kabisa hapa JF kukemea na kushauri uvurugaji wa uchaguzi husika.
Hata hivyo hatuna ushahidi kama ndio waliambiwa wakafanye hicho unachotuhumu, sikukatalii kama ni kweli au si kweli usemacho lakini nakuonesha bado hujathibitisha madai yako, yatabaki kuwa tuhuma.
 
Back
Top Bottom