Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Yaani hizi sifa za kijinga zitatusumbua vichwa bure. Yupi kati ya Gwajima na Makonda ana afadhari? Makond dhambi ya kumpiga kofi Warioba itakusumbua sana.
 
hivi kuna sheria gan inayomtaka mtu kwenda kujieleza kwa mkuu wa wilaya kama anavyotaka makonda na kwani Gwajima asipoenda kutatokea nini?.Naomba mnaojua mnisaidie kwa hili tafadhali
 
Makonda kuwa mwangalifu sana na imani za watu na hawa viongozi wa kidini huwa wanafuatwa kwenye makanisa/misikiti yao huwa hawaitwi.....wanaheshimiwa.
 
Alitumwa.ndo maana akapewa ukuu wa wilaya

Makonda mwehu yeye alipomtukana lowasa waziri mkuu na kumpga Jaji Warioba waziri mkuu mstaafu alirpoti huyu mwehu asome Sheria vizuri tatzo chuo ata mitihan alkua anafanyiwa kuwa mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama si kujigeuza polisi ajiulizi kwanini CDF hawezi kumuita mtu ofsni kwake kwa kutoa lugha chafu
 
Kama mlikuwa hamjui gwajima kamgusa mwenye nchi haya yaliyo mkuta gwajima ndio yaliyo mkuta ponda pengo ndio kiongozi katika nchi hii bora umtukane mkuu wa kaya kuliko pengo sisi ndio tunaujua mfumo kristo unavyo tawara nchi
 
Kichaa kapata RUNGU.Polisi wameshaanza mambo ya kisheria na wewe Makonda unaingilia je? Achia polisi wafanye kazi zao.Pia muite nayule aliye mkwita Waziri mkuu mstafu Warioba,wote walivunja sheria.
 
Kama mlikuwa hamjui gwajima kamgusa mwenye nchi haya yaliyo mkuta gwajima ndio yaliyo mkuta ponda pengo ndio kiongozi katika nchi hii bora umtukane mkuu wa kaya kuliko pengo sisi ndio tunaujua mfumo kristo unavyo tawara nchi

Udini umekijaa kwani gwajima sio mkristo???
 
ni jambo jema lakini wasiwasi wangu kusije kukawa na conflict of interest. mfano kama makonda ni mkatoliki au anaunga mkono katiba pendekezwa sidhani kama gwajima atatendewa haki hapo japo sikubaliani na uwendawazimu alioufanya gwajima. nadhani hili liachiwe vyombo vya sheria kama polisi na mahakama ili kulinda haki za watu.
Muvi inaendelea wakuu,

Wakati Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amejisalimisha kwenye Jeshi la Polisi kwa mahojiano hali iliyopelekea Askofu huyo kupoteza fahamu; naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka Askofu huyo aripoti ofisini kwake keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.


Makonda amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. "Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini."

11081016_360745177443838_2390948105818373976_n.jpg



 
Mkuu wa wilaya ni mlinzi wa amani kwenye wilaya yake.Matamshi ya Gwajima yaweza letelea vurugu katika wilaya yake ya kinondoni kati ya wakatoliki wanaomheshimu Pengo na wafuasi wa Gwajima waliokuwa wakishangilia wakati Pengo akiporomoshewa matusi ya nguoni.

HIVYO KUMWITA NI SAWA
makonda ni nani mpka amwite gwajima mlinzi wa amani wakati anamfanyia fujo warioba alikuwa nani una akili wewe tena wacha niishie hapo
 
Mlalamikaji katika hiyo kesi atakuwa nani?

Au ndio mwendelezo wa pengo kuwa askofu wa serikali?
Katika kesi zote za jinai mlalamikaji mkuu/complainant kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai ni serikali, muhanga kama Pengo kwa mfano anakuwa ni shahidi mkuu, hata ww kwa mfano ukipigwa mlalamikaji ni serikali ww utakuwa shahidi mkuu
 
Wapendwa nawashauri tupunguze maneno ya kashfa. Mungu kamwe hazihakiwi apandacho mtu ndicho atakachovuna. Kama ni mdomo umemponza Ask Gwajima je wewe unayemtukana unatumia nini?


Huko kwenye KANISA lake nasikia watu wamefunga KAVU wanaporomosha maombi ya kutosha. Sasa tuwe waangalifu maana hukumu ni ya Bwana.


Baba Ask Pengo ni mtumishi wa Mungu, siamini kuwa Leo wakristo tunalipana ubaya kwa ubaya (Kama upo). Hata mafarisayo walipomtukana Yesu, neno la Mungu linasema hakufunua kinywa chake. Ask Pengo ni kiongozi mwenye kufuata mfano wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tena imeandikwa ukipigwa shavu la kushoto, geuza na la pili...... Kesi ya wana wa Mungu lini ikaamuliwa na MATAIFA????? Eeeeee Mungu, nyosha mkono wako, wanadamu wanafanya ghasia juu ya watumishi wako. Eeeee Bwana ikikupendeza tuinulie mtumishi wako, nabii wa siku, kulimaliza kesi ya watoto wako ili injili iendelee kuhubiriwa. Kwa Jina la Yesu Kristo tumeomba. AMEN


Mwisho je,, Hawa wote wanaomshitaki Ask Gwajima wametumwa na Pengo (siamini). Kama wana vita yao na Ask Gwajima isipitie kwa baba yetu mpendwa Pengo. Anyway vita ya KIROHO siku zote humalizikia rohoni. Kwenye hili tuwe waangalifu sanaaaaaaaa!!!


Mwisho wale mnaojiita wakristo, tabia ya kukashifu dini ya mwenzio au kiongozi wa KANISA lingine sio nzuri kabisa. Mkumbukeni Mtume Paulo alipowajibu wale waliokuwa wamejimilikisha jina la Yesu kuwa... as long as Kristo anahubiriwa iwe kwa hila au..... jina la Bwana litukuzwe.


Tuendelee na maombi ya kuiombea nchi yetu changamoto ni nyingi, tuukomboe wakati, usiutie unajisi moyo wako.


Mungu atubariki na atusaidie.


Queen Esther

Ukristo hauruhusu unafki...anachokifanya pengo ni unafki na kama mkristo anakosea sana.hata yesu alikuwa na msimamo kwenye mambo ya Mungu...Pengo kila siku anatoa kauli tata ambazo kwa kiasi kikubwa anonekana kuelemea siasa za Chama Cha Mapinduzi.Kama kweli yeye ni mkristo safi asingekimbilia polisi angemuita Gwajima ili waeleweshane
 
Huyu dogo ana matatizo, si bure.
Kama jambo limeshafika katika ofisi ya jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam yeye aawezaje kuliingilia? Ukichukulia wote ni sehemu ya serikali na atakaowayumia kufanya law enforcement wapo chini ya kanda moja na jambo linaloshughulikiwa ni lile lile!!
 
makonda kawakamate waislam wa pale mbagala maana kila siku wao ni kusema wakristo makafir na mengine ambayo nashindwa kuyasema hapa.Achana na huyo askofu kuna kuna shtaka kafungue mahakamni,pengo mnafiki tu

Siku hizi Mbagala ipo Kinondoni au umepitiwa?
 
Back
Top Bottom