Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,116
- 8,652
Yaani hizi sifa za kijinga zitatusumbua vichwa bure. Yupi kati ya Gwajima na Makonda ana afadhari? Makond dhambi ya kumpiga kofi Warioba itakusumbua sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alitumwa.ndo maana akapewa ukuu wa wilaya
Kama mlikuwa hamjui gwajima kamgusa mwenye nchi haya yaliyo mkuta gwajima ndio yaliyo mkuta ponda pengo ndio kiongozi katika nchi hii bora umtukane mkuu wa kaya kuliko pengo sisi ndio tunaujua mfumo kristo unavyo tawara nchi
Muvi inaendelea wakuu,
Wakati Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amejisalimisha kwenye Jeshi la Polisi kwa mahojiano hali iliyopelekea Askofu huyo kupoteza fahamu; naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka Askofu huyo aripoti ofisini kwake keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.
Makonda amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.
Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. "Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini."
![]()
makonda ni nani mpka amwite gwajima mlinzi wa amani wakati anamfanyia fujo warioba alikuwa nani una akili wewe tena wacha niishie hapoMkuu wa wilaya ni mlinzi wa amani kwenye wilaya yake.Matamshi ya Gwajima yaweza letelea vurugu katika wilaya yake ya kinondoni kati ya wakatoliki wanaomheshimu Pengo na wafuasi wa Gwajima waliokuwa wakishangilia wakati Pengo akiporomoshewa matusi ya nguoni.
HIVYO KUMWITA NI SAWA
Tunataka viongozi wa namna hii safi sana makonda dc kijana mchapa kazi.
Katika kesi zote za jinai mlalamikaji mkuu/complainant kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai ni serikali, muhanga kama Pengo kwa mfano anakuwa ni shahidi mkuu, hata ww kwa mfano ukipigwa mlalamikaji ni serikali ww utakuwa shahidi mkuuMlalamikaji katika hiyo kesi atakuwa nani?
Au ndio mwendelezo wa pengo kuwa askofu wa serikali?
Wapendwa nawashauri tupunguze maneno ya kashfa. Mungu kamwe hazihakiwi apandacho mtu ndicho atakachovuna. Kama ni mdomo umemponza Ask Gwajima je wewe unayemtukana unatumia nini?
Huko kwenye KANISA lake nasikia watu wamefunga KAVU wanaporomosha maombi ya kutosha. Sasa tuwe waangalifu maana hukumu ni ya Bwana.
Baba Ask Pengo ni mtumishi wa Mungu, siamini kuwa Leo wakristo tunalipana ubaya kwa ubaya (Kama upo). Hata mafarisayo walipomtukana Yesu, neno la Mungu linasema hakufunua kinywa chake. Ask Pengo ni kiongozi mwenye kufuata mfano wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tena imeandikwa ukipigwa shavu la kushoto, geuza na la pili...... Kesi ya wana wa Mungu lini ikaamuliwa na MATAIFA????? Eeeeee Mungu, nyosha mkono wako, wanadamu wanafanya ghasia juu ya watumishi wako. Eeeee Bwana ikikupendeza tuinulie mtumishi wako, nabii wa siku, kulimaliza kesi ya watoto wako ili injili iendelee kuhubiriwa. Kwa Jina la Yesu Kristo tumeomba. AMEN
Mwisho je,, Hawa wote wanaomshitaki Ask Gwajima wametumwa na Pengo (siamini). Kama wana vita yao na Ask Gwajima isipitie kwa baba yetu mpendwa Pengo. Anyway vita ya KIROHO siku zote humalizikia rohoni. Kwenye hili tuwe waangalifu sanaaaaaaaa!!!
Mwisho wale mnaojiita wakristo, tabia ya kukashifu dini ya mwenzio au kiongozi wa KANISA lingine sio nzuri kabisa. Mkumbukeni Mtume Paulo alipowajibu wale waliokuwa wamejimilikisha jina la Yesu kuwa... as long as Kristo anahubiriwa iwe kwa hila au..... jina la Bwana litukuzwe.
Tuendelee na maombi ya kuiombea nchi yetu changamoto ni nyingi, tuukomboe wakati, usiutie unajisi moyo wako.
Mungu atubariki na atusaidie.
Queen Esther
makonda kawakamate waislam wa pale mbagala maana kila siku wao ni kusema wakristo makafir na mengine ambayo nashindwa kuyasema hapa.Achana na huyo askofu kuna kuna shtaka kafungue mahakamni,pengo mnafiki tu
Paul Makonda huyu-huyu aliyemtandika makofi Jaji Warioba??
Yaani hizi sifa za kijinga zitatusumbua vichwa bure. Yupi kati ya Gwajima na Makonda ana afadhari? Makond dhambi ya kumpiga kofi Warioba itakusumbua sana.