Paul Makonda apewe Ubalozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati au Burundi?

Paul Makonda apewe Ubalozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati au Burundi?

Bashite ni swala la muda tu aingie kwenye list ya intapol akashtakiwa marekani kwa mauaji ya kimbari. Nafikiri mama fadhila zitamponza
Teh ndo wamewatuma hivyo mabwana zenu,,,,hayo kafanyeni kenya sio huku
.....kete za huku hamziwezi
 
Teh ndo wamewatuma hivyo mabwana zenu,,,,hayo kafanyeni kenya sio huku
.....kete za huku hamziwezi
Endelea kufadhiliwa condom, neti za mbu, dawa za malaria na ARV kwa msaada wa watu wa marekani
 
mi nadhani apelekwe Israel akawe mpatanishi wa Israel na waparestina nakuhakikishia popote atakakopelekwa atafaa tu kwa sababu ana maono kwa kile anachofanya. naona mnaweweseka mnaanza hata kuogopa kivuli chake kwa taarifa yako akigombea ubunge akapita tumhesabu kwenye uwaziri mkuu atawanyosha kwelikweli
 
Endeleeni kuwalamba miguu maana bila hao hamuendi chooni na familia zenu
Hahaahaha bila msaada wa mabeberu hupumui nchi hii kama hujui pesa za miradi ya maendeleo zote za mabeberu poleni jiwe aliwadanganya
 
Hahahahah sukuma gang hamna future msoga wamepenya kwa mama

View: https://twitter.com/mangekimambi/status/1797034713607274959?t=NQTbMbSrbq8fOfYDnC2nbw&s=19

We Zombi
Screenshot_20240602-134641_X.jpg
Screenshot_20240602-134629_X.jpg
 
Salaam Wakuu,

Kwa kuwa ameonekana kutokukubaliana na Sera za Rais Samia, alitakiwa ajiuzulu bila Shuruti.

Paul Makonda ni Mwenezi wa CCM na Samia Suluhu ni Mwenyekiti. Mwenezi hakubaliani na Mwenyekiti, anatakiwa aachie ngazi kuliko kutengeneza mtatandao wa matajiri kwa nia Ovu.

Siku zote Rais Samia amesema Serikali yake ni awamu ya Sita. Makonda anasema Serikali ni ya awamu ya tano sababu inatumia Ilani ya awamu ya tano. Je, anabishana na Rais wake?

Kuna maneno anaongea kumkejeli mtu aliyemteua kana kwamba hajui kazi. Mfano anasema "Nabadilika kutokanana Mazingira, Ningeteuliwa kipindi cha Magufuli Chuma, wale jamaa wangenyooka - unatamani kupiga panchi onaona Mama sio Mapigo yake" Hizi ni dharau kwa rais. Kwamba Samia sio Chuma? Wakati kakupa uteuzi?
View attachment 2945836
Kwa nafasi yake ya Uenezi anasema tusimtofautishe Rais Samia na Hayati Magufuli. Kwanini anakataa tusimtofautishe wakati tofauti zinaonekana?

1. Rais Samia Kaunganisha Nchi wakati Magufuli aliisambaratisha

2. Rais Samia kafungua Nchi kipindi cha Magufuli tulikuwa kama Kisiwani

3. Rais Samia hakuna Utekaji wala watu kupotea kipindi cha Magufuli tulikuwa tunaokota Maiti kwenye zimefungwa kwenye Gunia zikielea Coco beach.

4. Rais Samia hanyang'anyi pesa za mtu zilizopo Benki, kipindi cha Magufuli alikuwa anatuma watu wakague mabenki nani ana fedha nyingi kisha wanamfungulia kesi ya Uhujumu Uchumi baadaye anawataka wagawane hela zilizopo Benki ili wawe huru

5. Rais Samia karuhusu Mikutano ya Siasa, Kipindi cha Magufuli hapakuwa na Mkutano ya siasa

6. Rais Samia anatupa tume huru wakati wa Magufuli alikuwa anaengua watu na Wagombea wa Vyama vya upinzani wanafungwa jela wakitoka CCM ishashinda.

7. Tais Samia yupo kwenye Mchakato wa kutupa Katiba Mpya, Wakati wa Magufuli alisema haliitangaza kwenye ilani ya CCM.

Yapo mengi sana.. Sasa hivi Watanzania wanafuraha na wqnatabasamu nk.

Halafu Makonda anatokea huko eti Magufuli na Samia ni kitu kimoja.

Paul Makonda anadanganywa na Polepole. Nia yake ni kumtoa Rais Samia kwenye reli.

Alichukua hela za matajiri, kaenda kufanya Mikutano kanda ya Ziwa ili kumtisha Mama kwamba bila Makonda Samia hapati kura. Anajidanganya.

Ni wakati wa Samia kumpangia kazi nyingine. Sababu ubalozi wenyewe alishapigwa ban kwenda Marekani wala kuhudhuria Mikutano inayoongozwa na Marekani kwa kosa la kudhurumu uhai wa binadamu alipokuwa Mkuu wa Mkoa.

Makonda ni Jumba bovu. Asimuangukie Rais wetu bado tunamtegemea. Alituvusha salama kipindi cha Msiba wa Taifa na Bado Kasimama.

Makonda asimchafue. Amuache awaletee maendeleo Watanzania. Asilinganishwe na yoyote
ukimpa ubalozi hizo nchi si atavamia kazi za raisi wa hizo nchi
 
Mpeleke tangulia fasta
Tatizo ni hizo Mahakama za CCM zinazofunga Wezi wa Kuku na kuyaacha Mafisadi.

Mike Pompeo alisema Makonda anawanyima Watanzania HAKI YA KUISHI weye unajua maana yake?!
 
Tatizo ni hizo Mahakama za CCM zinazofunga Wezi wa Kuku na kuyaacha Mafisadi.

Mike Pompeo alisema Makonda anawanyima Watanzania HAKI YA KUISHI weye unajua maana yake?!
Kanye boga
Screenshot_20231102_120808_Remix.png
 
Back
Top Bottom