Updates...
Kumepita ukimya wa takribani mwezi mmoja huku swali kuu likiwa yupo wapi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, RC Paul Makonda lakini leo Agosti 16, 2024 swali hilo limejibiwa baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza akikagua ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Arusha uliopo eneo la Kisongo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Mkoa Arusha na kukagua Ujenzi huo unaondelea kutekelezwa leo Agosti 16, 2024 ameeleza chanzo cha utanuzi wa Uwanja huo.
RC Makonda amelezea kuwa itakuwa chanzo cha utanuzi kwa Uwanja huo wa ndege ni kuongeza kundi kubwa la Watalii wanaoingia nchini kupitia mkoa wa Arusha kwa uwepo wa vivutio mbalimbali vya utalii ambapo itaongeza Uchumi kwa taifa letu na kujitangaza zaidi kupitia utalii.
RC Makonda ameeleza zaidi kuwa ifikapo Septemba Mosi Uwanja kuanza kutumika kuanzia Septemba mosi, 2024 ambapo idadi ya watalii inakadiriwa kuongezeka zaidi.
Mkandarasi
Moja ya Miradi ambayo itafanyika katika uwanja huyo wa ndege ni kufunga taa za kuongozea Ndege kwa sababu uwanja wa ndege uwe kufanya kazi masaa 24.
"Tumeshapata Mkandarasi tayari na tumeshamkabidhi na sasa yupo katika hatua ya kufanya usanifu wa mfumo wenyewe".
"Lakini tatizo ambalo tunalo ni hile ardhi ya kufunga hizo taa za aproch ya kutua ndege, kwa sababu kiwanja chetu kutoka pale mwisho tuna mita 200 na lakini tunahitaji mita 500".
Soma Pia: Bananga: Jana nimeongea na Makonda sasa yupo Arusha, amemaliza likizo yake