Paul Makonda arejea, aibukia Uwanja wa Ndege Arusha uliopo eneo la Kisongo

Paul Makonda arejea, aibukia Uwanja wa Ndege Arusha uliopo eneo la Kisongo

Wao waimarike tu maana unadhani bila CCM hizi Ng'ombe za Tanzania nani atazichunga!?
Mkuu yaani sisi tumegeuka Ngombe tena, laah ila yawezekana ikawa kweli eee - yaani tunaswagwa tu hatujui tutokapo wala tuendako.
 


Updates...

Kumepita ukimya wa takribani mwezi mmoja huku swali kuu likiwa yupo wapi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, RC Paul Makonda lakini leo Agosti 16, 2024 swali hilo limejibiwa baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza akikagua ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Arusha uliopo eneo la Kisongo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Mkoa Arusha na kukagua Ujenzi huo unaondelea kutekelezwa leo Agosti 16, 2024 ameeleza chanzo cha utanuzi wa Uwanja huo.

RC Makonda amelezea kuwa itakuwa chanzo cha utanuzi kwa Uwanja huo wa ndege ni kuongeza kundi kubwa la Watalii wanaoingia nchini kupitia mkoa wa Arusha kwa uwepo wa vivutio mbalimbali vya utalii ambapo itaongeza Uchumi kwa taifa letu na kujitangaza zaidi kupitia utalii.

RC Makonda ameeleza zaidi kuwa ifikapo Septemba Mosi Uwanja kuanza kutumika kuanzia Septemba mosi, 2024 ambapo idadi ya watalii inakadiriwa kuongezeka zaidi.

Mkandarasi
Moja ya Miradi ambayo itafanyika katika uwanja huyo wa ndege ni kufunga taa za kuongozea Ndege kwa sababu uwanja wa ndege uwe kufanya kazi masaa 24.

"Tumeshapata Mkandarasi tayari na tumeshamkabidhi na sasa yupo katika hatua ya kufanya usanifu wa mfumo wenyewe".

"Lakini tatizo ambalo tunalo ni hile ardhi ya kufunga hizo taa za aproch ya kutua ndege, kwa sababu kiwanja chetu kutoka pale mwisho tuna mita 200 na lakini tunahitaji mita 500".

Soma Pia: Bananga: Jana nimeongea na Makonda sasa yupo Arusha, amemaliza likizo yake

Kazi kazi ma meeen...yaani huyu mwamba chuga ataieshimisha mnoo
Nyie makolo weche chuki za kisiasa
Bakini na chuki zenu maisha yanaendelea
 
Ibada zetu zinaongozwa na yaliyomo kwenye vitabu vyetu vitakatifu. Waislam wanaswali mara 5 kwa siku na swala zao hizo ni fupifupi tu dk 5 wakati anasubiri au anashuka kwenye ndege. Wakristo huwa wanasali siku za jumapili au jmosi tu, hivyo huhitaji kuweka kanisa ndani ya airport hapo ambalo halitatumika. sio kila kitu kinahitaji kubalance.

Tuache viwango vya kimataifa vitumike, na tuwaache wahandisi na michoro na ramani ifanye kazi, vinginevyo hakuna siasa hapo kwenye kila kitu


View: https://www.youtube.com/watch?v=IHztQrYAF0g
 
L
Ibada zetu zinaongozwa na yaliyomo kwenye vitabu vyetu vitakatifu. Waislam wanaswali mara 5 kwa siku na swala zao hizo ni fupifupi tu dk 5 wakati anasubiri au anashuka kwenye ndege. Wakristo huwa wanasali siku za jumapili au jmosi tu, hivyo huhitaji kuweka kanisa ndani ya airport hapo ambalo halitatumika.

Tuache viwango vya kimataifa vitumike, na tuwaache wahandisi na michoro na ramani ifanye kazi, vinginevyo hakuna siasa hapo kwenye kila kitu


View: https://www.youtube.com/watch?v=IHztQrYAF0g

Lakini pia ni kitu kizuri! Maana mtu anaweza kuhitaji kutulia kwa maombi yake binafsi! Lakini pia usidanganye watu hapa kuwa Wakristo wanasali jumamosi na jumapili tu!
 
Back
Top Bottom