Pre GE2025 Paul Makonda: Arusha hawakupata barabara kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwahiyo wilaya za Geita tena zenye madini hazina barabara, maji safi, umeme na zinachagua CCM kila siku nazo tusemeje
 
Ulishawahi ishi arusha sababu unabisha ujinga

Double road ya kwanza arusha imejengwa wakati lema akiwa mbunge tokea tengeru mpaka sakina
Acha uyanani ,hii barabara ipo kwenye mipangonya serikali hadi himo holili na sio Lema aliepiga debe hadi ikajengwa
 
Dodoma hakuna jimbo hata moja la upinzani ila kuna miundombinu mibovu kupita maelezo same kwa ruvuma, lindi, na mikoa mingi
Jamaa Hana akili kabisa ataweza kufanya hiyo analysis?
Tusahau maendeleo kama ndio viongozi wetu hao wanawaza namna Hii.
 

Basi nenda kawashauri CCM wafanye marekebisho ya Katiba ili kuruhusu Tanzania iwe na mfumo wa chama kimoja. Ukishasema mfumo wa vyama vingi basi Ina maendeleo yatatolewa kwa wananchi bila kuangalia vyama wanavuounga mkono.
 
Huyo zero brain hajui kuwa barabara nzuri zinatokana na kodi za wananchi.?

Watu wanalipa kodi wao wanaenda kuzitapanya kwenye Kizimkazi festival na kununua magoli wanafikiria nini?

Hapo kosa ni la wananchi au serikali isiyo na vipaumbele?
 
Hivi majungu ya wanasisa wachache katika mkoa yanaweza kuwa ndiyo kigezo cha kuwanyima walipa kodi maendeleo?
 
Basi nenda kawashauri CCM wafanye marekebisho ya Katiba ili kuruhusu Tanzania iwe na mfumo wa chama kimoja. Ukishasema mfumo wa vyama vingi basi Ina maendeleo yatatolewa kwa wananchi bila kuangalia vyama wanavuounga mkono.
Hakuna haja ya chama kimoja ila ni Vyama vingi,watakaoshunda ndio wataamua wapi Wapeleke pesa bila kujalisha wamezikusanya wapi maana wengi wape wachache watafanyiwa uungwana ila hawana maamuzi.

Unapochagua Wapinzani na huwezi shika Serikali umejitumbukiza shimoni ukisubiria huruma ya aliyeshika Dola ,ndio kanuni ya Demokrasia πŸ˜„πŸ˜„
 
Dodoma hawajawahi chagua upinzani huko ni ccm mwanzo mwisho mbona kuna umaskini wa kutisha same kwa ruvuma na lindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…