Paul Makonda: Arusha sasa inazalisha Magari aina ya Defender na kuyapeleka Ulaya

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameweka wazi kuwa Arusha imeanza kutengeneza magari aina ya Defender, ambayo sasa yanauzwa Ulaya. Akizungumza kwenye kongamano la Radiolojia lililofanyika leo Oktoba 9, jijini Arusha mbele ya Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko, Makonda ameeleza kuwa magari hayo yanatengenezwa moja kwa moja jijini Arusha na kusafirishwa hadi Ulaya.

"Defender sasa zinanunuliwa kutoka Arusha, zinatengenezwa hapa na kisha kupandishwa meli kupelekwa Ulaya."

Kwakweli huu ni uongo
Ni kweli,kama umeona wimbi la Landrover defender mtaani ambazo zimekuwa pimped,hizo zinatengenezwa Arusha,wanachukua zulizotumika au chakavu wanazifanyia ukarabati wa nguvu zinakuwa kama mpya kabisa
Landrover.jpg
...
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameweka wazi kuwa Arusha imeanza kutengeneza magari aina ya Defender, ambayo sasa yanauzwa Ulaya. Akizungumza kwenye kongamano la Radiolojia lililofanyika leo Oktoba 9, jijini Arusha mbele ya Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko, Makonda ameeleza kuwa magari hayo yanatengenezwa moja kwa moja jijini Arusha na kusafirishwa hadi Ulaya.

"Defender sasa zinanunuliwa kutoka Arusha, zinatengenezwa hapa na kisha kupandishwa meli kupelekwa Ulaya."
Na yeye amekubali hizo fix🤣
 
Back
Top Bottom