Paul Makonda: Arusha sasa inazalisha Magari aina ya Defender na kuyapeleka Ulaya

Paul Makonda: Arusha sasa inazalisha Magari aina ya Defender na kuyapeleka Ulaya

Hata uwe na akili vipi, ukiongozwa na mjinga tu basi nawe ni PIMBI, watanzania sisi ni ma.................................. 😂🤣
 
Huyu itakuwa anamaanisha zinafanyiwa repair au facelift...sio uundaji wa gari tokea kukunja chuma n.k
Hata hiyo face lift ndio kweli watu watoke Ulaya kuja kununua gari Arusha?? Waache face lift za kina Khan Design?
 
Nadhani wengi hamjamuelewa. Kuna tofauti kubwa kati ya car manufacturing n car assembly. Alichosema blaza Paulo ni uhalisia kwa 100%. Nilipata nafasi ya kuitembelea kampuni ya uzalishaji wa mabasi 0 mileage pale ke, "Master Fabricators." Arusha kuna car assembly ya madefenda. Car assembly inanunua spare parts nje, then inategeneza gari jipyaaa. Kwa sasa nchi za kiafrika almost wote tumejikita kwenye car assembly maana bado hatuna uwezo wa kuzalisha spare parts zetu.
Wengi wamejaa makasiriko. Ukiweka na chuki zao juu ya Makonda chochote atakachosema povu linawatoka. Hizo Defender sasa hivi zishakuwa DISCONTINUED hazitengenezwi kabisa na JLR. Kinachofanyika duniani ni watu independent wanasuka zile za zamani zinakuwa na features za kisasa. Arusha napo wanafanya hivi, wanachukua scrapper kabisa hata halitembei wanaweka kila kitu kipya hadi chassis na sehemu za body. Hio ni assembly kabisa. Replacement ya OG Defender ni Ineos Granadier ambay ni kampuni tofauti na JLR.
 
Tukiachana na uongo wa Makonda naomba kuuliza kama kuna namna yoyote wanafaidika kwa kuipa Land Rover promo kubwa kiasi hicho? Hatuoni kama Land Rover wanatuona wajinga kuwapa matangazo ya bure? Itachukua muda sana kwenda sawa na ulimwengu wa kibepari.
Ndio uwaambie jamaa zako wa CCM,mnakuja taratibu na Mwashambwa!
 
Nimezikuta land cruiser zilizobadilishwa muundo (alteration) na kuongezwa urefu Arusha au Moshi, zipo Saudi Arabia. Kuna Saudi alizoiona Arusha akaona fursa hii, anaziuza kwa order huko Saudi Arabia. Ana order huyo, hazitoshi, sijuwi singa gani wa Arusha ndiyo anaziunda hivyo.
 
Back
Top Bottom