Uchaguzi 2020 Paul Makonda: Asanteni sana Kigamboni, mapenzi ya Mungu ni makubwa kuliko mapenzi yangu

Uchaguzi 2020 Paul Makonda: Asanteni sana Kigamboni, mapenzi ya Mungu ni makubwa kuliko mapenzi yangu

Hizo connection ni za kinafiki, walimpenda akiwa kwenye kiti sahivi hana kiti nani atamuangalia, wanadamu umewasahau ehh
Connection kama GSM, IGP, Mambosasa, Magufuli obviously siyo wajumbe pale Kigamboni.
 
Kwanza nimpe pole Makonda kwa matokeo ya jana!

But I’m confused, “Asanteni....na kunipa nafasi niwe sehemu ya Maisha yenu”. Is he in denial?
Kura 122 siyo nafasi? Be serious!
 
Ccm bado hawajaweka usawa ktk hii michakato ya kura za maoni.

Unajua unapokuwa kakikundi eti ka kamati ya siasa ni rahisi sana kukafanyia robbing.

Hii ilitakiwa kila kijiji wanachama wte wa ccm wapige kura.


Ikiwa hivyo itakuwa ngum sana mgombea kuwahonga wanachama wte kila kijiji ktk jimbo lote.
Hata km amepewa mafao hawezi kuwahonga wte.
Lakini hii stail nirahisi sana kuaanda kikundi chako kuanzi kipindi cha wagombea kura za ujumbe wa kamati za siasa kijiji.

Naamini wengi walopita hasa wabunge walomaliza mda wao %kubwa walitembeza njugu be4.
Lobbying na sio robbing.
 
ANAWATAKIENI BARAKA...very very pathetic

“Nimepata pole nyingi sana kutokana na matokeo ya jana, kwanza nawashukuru kwa upendo wenu na maombi yenu ya kunitakia mafanikio katika kutimiza NDOTO yangu”

“Jambo moja kubwa ni muhimu ni kuyajua mapenzi ya Mungu na katika hili mapenzi ya Mungu ni makubwa kuliko mapenzi yangu, nawatakia baraka na afya njema siku zote za Maisha yenu, Asanteni sana sana Wana KIGAMBONI kwa upendo wenu na kunipa nafasi niwe sehemu ya Maisha yenu”
 
kushiriki mchakato kura za maoni kunajenga CV na kuonesha wakubwa uko fit na huogopi mikuki!! manake siasa zetu ni za majitaka chafua nikuchafue nani hana skendo??! nani msafi?

Ikumbukwe kuwa Bashite jumba bovu limemuangukia kwa ujeuri na ufedhuli wake wa kudharau position kubwa aliyopewa na Mungu kupitia Mr Mubashara wekeni kira kitu raiv bira chenga!! Nao Mzee kijana Slow times two na Katibu mkuu waliapa kunyoosha kina Bashite na Mnyeti walioasi!! tusubiri!!

Bashite kusema ukweli amefanya vyema kushukuru watu wake wa kufikia Kigamboni maana yeye ni wa Kolomije alikopaswa kwenda kugombea , Bashite kushukuru ni muungwana!

Makonda ni mtu mshamba aliebaki na kijiji kichwani mwake na hata alipopewa mamlaka makubwa yakamlevya akasahau cheo cha uhudumu wa umma ni dhamana! huwezi kujilinganisha na MO Dewji au mtoto wake wao vyeo si dhamana!!

Makonda alipaswa kuwania jimbo la Ukonga ambalo halina mwenyewe sababu hata mbunge wake Waitara raia hawamjui na hawataki kumsikia sababu hufika mara moja tena siku ya kampeni na hajawahi kuzungumzia matatizo ya ukonga bungeni zaidi ya harakati zake za kuikosoa sirikali tu akiwa mwana Chadema!!

Makonda lazima kama ni mwanaume kweli akae chini atafute alikosea wapi kuchanga karata zake japo mimi najua kuna watu wa karibu waliomuingiza choo cha kike lazima awatambue!! Alipaswa kuanzia chini jimbo dogo lisilo na ushindani mkubwa! Makonda tunajua alikimbilia Kigamboni kwa tamaa ya madili ya ardhi na uwekezaji, tamaa imemponza!!

Watu wa Ukonga wanamtaka Makonda kwa udi na uvumba, wanasema ni mtu mpenda sifa na kiki na akiwa mbunge wao atafanya mengi kutafuta sifa nao wataendelea, , ukonga Goms kuelekea Machokoroni huko Majohe, Viwege, Mvuti, Chanika, Nzasa , Mbande na Masaki wanamuomba Mh Rais angempa viti Maalum Makonda kudeal na jimbo la Ukonga , iwe wilaya mpya Gongo la Mboto all the way to Nzasa!!

tukumbuke yeye Makonda ni mwanadamu njia yake anayo Allah japo sote tungependa kumuona akirudi Mwaloni kugaa gaa na upwa but watu wa Ukonga wanasema hiyo Dhahabu mmeikataa Kigamboni tuleteeni Ukonga sababu eti Makonda anapenda sifa maendeleo yangepatikana makubwa hadi taa za barabarani usiku zingewekwa, double Road Goms to Nzasa, hospital kubwa hakuna , umeme hukatika huko ukonga kwa siku mara tatu!!

Kama kuna kitu anapaswa kufanya Makonda kwasasa ni kwenda Ukonga wanakomtaka akajiegemeze huko, kigamboni town sana wajanja wengi, Ukonga washamba wageni na wahuni kibao halafu kila mtu na time yake hakuna umoja wala discussion kati ya mtu mmoja na mwingine!!
 
mapenzi ya Mungu ni makubwa kuliko mapenzi yangu
Asome Bible Vizuri, mapenzi ya Mungu yanakamilishwa in Christ Jesus, Mapenzi ya Mungu ni Kutaka watu wote waokolewe( Asome Timoth Yote)
Hakuna Mapenzi ya Mungu nje ya hapo.
 
Back
Top Bottom