Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

Kuna watu sijui sura zao wataweka wapi. Walifanya makosa yale yale waliyomtukania Makonda kwa kumbagaza bila kujua kesho yake. Tulivyo wanafiki kama Mungu angetuonesha kesho ya Makonda wala wasingemtukana.

Subiri muone sasa wasanii, mastar na wanasiasa watavyorejea kujipendekeza!

Hongera sana Paul Makonda, toka 2021 - 2023 ulikuwa chuoni naamini umehitimu sasa.
Hahahah marehemu lemutuz angekuwepo sijui angejificha wapi
 
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 22 Oktoba, 2023 mjini Dodoma, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Dokta Samia Suluhu Hassan, pamoja na masala mengine, imeridhia kwa kauli moja na kuielekeza Serikali kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendelezaji na uwekezaji wa bandari.

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwa kumteua Ndugu Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya Ndugu Sophia Edward Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masala ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum.


Halmashauri Kuu ya CM Taifa pia imemteua Ndugu Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), akichukua nafasi ya Ndugu Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki.

Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dokta Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.

View attachment 2789088
Hapo Chichiem mumepatia kuna watu jumapili hii itakuwa ngumu Sana kwao
 
Inategemea rais nani? Kama mama huyu mwenye huruma Makonda ataishia kujenga hoja. Mama ana huruma sana
Maza alimkingia kifua asishughulikiwe...
Jamaa alipata malalamiko sana kutoka kwa Wahindi.. Walienda pale PCCB Upanga..
Wahindi walichotwa sana na Bashite...

Ila safari hii sidhani kama ataleta ubabe tena wa kiMagufuli
 
Back
Top Bottom