Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

View attachment 1342730
View attachment 1342609
Serikali ya Marekani imemzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingi nchini humo kutokana na kuhusika kwake kwenye uvunjifu wa Haki za Binadamu unaohusisha kunyima haki ya kuishi, uhuru na ulinzi wa watu.
Katika uongozi wake, Makonda ameonesha uonevu kwa wapinzani, kuminya uhuru wa kujieleza na kukusanyika na matendo maovu dhidi ya makundi maalum.
Marekani ina hofu kuhusu uvunjifu wa Haki za Binadamu na kupuuzwa kwa utawala wa sheria nchini Tanzania.
Kifungu namba 7031(c) kinampa uwezo Waziri wa Mambo ya nje kuweka zuio kama hili endapo mhusika amefanya ufisadi mkubwa au uvunjifu wa Haki za Binadamu. Pia kinamruhusu kuweka zuio kwa familia yake hivyo mke wa Makonda, Bi. Mary Felix Massenge amezuiwa pia.
Serikali ya Marekani inaikumbusha Serikali ya Tanzania kuheshimu utawala wa Sheria na Haki za Binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza na kukusanyika.
View attachment 1342609
Asanteeni sana USA

Hali ya haki za binadamu isipobadilika hapa nchini ni vema mkatoa kabsa economic sanction kwa Tanzania nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUJITEGEMEE,
Umeuliza. Jibu ni hili hapa chini.

Sisi tunaye mbabe wetu ambaye nasi tunayo orodha ya mambo mengi tunayolalamika juu yake. Lakini tunajua ni mbabe, na hatuna njia ya kumfanya lolote juu ya ubabe wake.

Huyo uliyemuorodheshea mambo hapo juu, na yeye ni Mbabe zaidi hata kumshinda huyu tuliyenaye sisi.
Bila shaka hadi hapo swali lako limejibiwa.
 
Crimea,
Kuna tofauti kubwa sana na hao uliowataja; kama huoni tofauti hiyo wewe utakuwa ni kipofu.

Pamoja na ubovu wao wote, ambao ndio unaoigwa na huyu unayemtetea, wenzake hao hawajawahi kuwashiwa taa yenye mwanga mkali kama huu aliowashiwa huyu wa kwako.

Ukitaka umdanganye akaze zaidi ukandamizaji wake wakati huu, hapo ndipo utakuwa umemchimbia kaburi lake moja kwa moja.
Akitaka kuwa na ahueni, mwambie awe mpole sana wakati huu kwenda mbele. Akitafuta kufurukuta ndio atakuwa anajimaliza.
 
Wazuie viongozi wote, pia Na sisi tuwawekee vikwazo viongozi wao
 
Hii ni kweli kabisa na ni habari ya moto. Ni shida yani
Aisee kweli boss,na kuna habari nimeiona imepostiwa humu jukwaani sijui kama ni ya kweli au la.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa raia wa Tanzania wamepigwa marufuku kushiriki katika mchezo wa bahati nasibu wa kupata viza ya kuingia Marekani.

Bahati nasibu hiyo hutoa visa kwa watu takribani 50,000 kutoka nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na kufanya kazi Marekani.

Nchi ya Sudani pia imepigwa marufuku kuingia katika bahati nasibu hiyo.

Kwa upande mwengine, raia wa nchi nne ikiwemo mbili za Afrika Nigeria na Eritrea wamepigwa marufuku kabisa kuomba viza za kuhamia Marekani.

Marufuku hiyo pia itazihusisha nchi za Myanmar na Kyryzstan.

Hata hivyo raia wa nchi hizo ambao watataka kuingia Marekani kwa kutalii ama biashara wataruhusiwa

BBC.

dodge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Le mutuz na yeye apigwe marufuku kuingia America kwani alikuwepo kwenye vx lililosimama getini kule Dodoma wakati Tundu Lisu akishambuliwa kwa Risasi na nyaulingo na kikundi chake cha akina kisanduku cyprian Musiba na wenzao, wote wapigwe marufuku kuingia hapa Marekani milele.
Hivi hilo kubwa jingwa bado lipo dunia hii
Ni muda mrefu sana halisikiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa wamempa umaarufu na mtaji mkubwa wa kisiasa Makonda.
Makonda sio waziri na kazi zake hazina umuhimu wa kwenda Marekani.

Hawezi kufa kwa kushindwa kuingia Marekani, kama ana fedha ataenda kutibiwa Ulaya au India na China, anaweza kuita madaktari bingwa toka Marekani na wakamhudumia hapa hapa Tanzania.
Zaidi ya 98% ya watanzania wanakufa kabla hawajatoka nje ya Tanzania kwenda Marekani au nchi jirani za EAC.
That's beside the point.

Wewe umeangalia upande huo uliokupendeza zaidi, ukasahau ujumbe mhimu uliowasilishwa!
 
kunyooshewa kidole na marekani ni kutafuta balaa, tumuombe Mungu ainusuru nchi.
 
Back
Top Bottom