Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Asanteeni sana USA

Hali ya haki za binadamu isipobadilika hapa nchini ni vema mkatoa kabsa economic sanction kwa Tanzania nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUJITEGEMEE,
Umeuliza. Jibu ni hili hapa chini.

Sisi tunaye mbabe wetu ambaye nasi tunayo orodha ya mambo mengi tunayolalamika juu yake. Lakini tunajua ni mbabe, na hatuna njia ya kumfanya lolote juu ya ubabe wake.

Huyo uliyemuorodheshea mambo hapo juu, na yeye ni Mbabe zaidi hata kumshinda huyu tuliyenaye sisi.
Bila shaka hadi hapo swali lako limejibiwa.
 
Crimea,
Kuna tofauti kubwa sana na hao uliowataja; kama huoni tofauti hiyo wewe utakuwa ni kipofu.

Pamoja na ubovu wao wote, ambao ndio unaoigwa na huyu unayemtetea, wenzake hao hawajawahi kuwashiwa taa yenye mwanga mkali kama huu aliowashiwa huyu wa kwako.

Ukitaka umdanganye akaze zaidi ukandamizaji wake wakati huu, hapo ndipo utakuwa umemchimbia kaburi lake moja kwa moja.
Akitaka kuwa na ahueni, mwambie awe mpole sana wakati huu kwenda mbele. Akitafuta kufurukuta ndio atakuwa anajimaliza.
 
Wazuie viongozi wote, pia Na sisi tuwawekee vikwazo viongozi wao
 
Hii ni kweli kabisa na ni habari ya moto. Ni shida yani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hilo kubwa jingwa bado lipo dunia hii
Ni muda mrefu sana halisikiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
That's beside the point.

Wewe umeangalia upande huo uliokupendeza zaidi, ukasahau ujumbe mhimu uliowasilishwa!
 
kunyooshewa kidole na marekani ni kutafuta balaa, tumuombe Mungu ainusuru nchi.
 
Upuuzi mtupu..Trump kabanwa sasa anatafuta pa kutokea...inaonekana ile movie ya Iran haikuwasaidia kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa hiyo unataka kusema hii ya Makonda aka X_house boy wa Mh Samwel Sita ndio itamsaidia Trump kutoka kisiasa? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mkuu unachekesha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…