Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Mh! Haya kazi kwenu majilani mliojenga nyumba za nyasi muwe makini msiuchezee moto
Sasa tunaelekea rasmi kuwa Taifa linaloruhusu Ushoga, ambao watetezi wake ni Zito, Fatma karume na Maria Sarungi.
 
Kumekucha sasa
Serikali ya Marekani imemzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingi nchini humo kutokana na kuhusika kwake kwenye uvunjifu wa Haki za Binadamu unaohusisha kunyima haki ya kuishi, uhuru na ulinzi wa watu.

Katika uongozi wake, Makonda ameonesha uonevu kwa wapinzani, kuminya uhuru wa kujieleza na kukusanyika na matendo maovu dhidi ya makundi maalum.

Marekani ina hofu kuhusu uvunjifu wa Haki za Binadamu na kupuuzwa kwa utawala wa sheria nchini Tanzania.

Kifungu namba 7031(c) kinampa uwezo Waziri wa Mambo ya nje kuweka zuio kama hili endapo mhusika amefanya ufisadi mkubwa au uvunjifu wa Haki za Binadamu. Pia kinamruhusu kuweka zuio kwa familia yake hivyo mke wa Makonda, Bi. Mary Felix Massenge amezuiwa pia.

Serikali ya Marekani inaikumbusha Serikali ya Tanzania kuheshimu utawala wa Sheria na Haki za Binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza na kukusanyika.

View attachment 1342609


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yatakuwa maajabu ya 8 ya dunia yaani pompeo atumie muda wake kabisa aandike kuhusu bashite-utakuwa anafanya upumbavu wa karne na kujiaibisha.
Wewe ndio unajiaibisha kwa kuonyesha ignorance yako hapa, kama haujui sio lazima uongee, nyamaza.
 
Kiukweli hawa mabeberu Wamarekani ni washenzi sana!, Wanamuonea bure Makonda tena kwasababu safari za Makonda US ni safari binafsi za yale mambo ya kifamilia, kumzuia Makonda kuingia US ni ukiukwaji wa haki ya msingi ya binaadamu.

Wito kwa Rais Magufuli, toa waraka hakuna kiongozi yoyote wa serikali yako ataomba Visa kuingia US, wanataka kutudhalilisha tuu, kwani Marekani ndio nini?. Twende China!.
To hell with America!.
Let's say no to American with their filthy blood stained, stinking money except " kwa msaada wa watu wa Marekani" zikiwemo ARV.
P
Pale viungo vya kukalia na vyakutolea Haja vinapotumika kufikiria na kuongea
 
Yatakuwa maajabu ya 8 ya dunia yaani pompeo atumie muda wake kabisa aandike kuhusu bashite-utakuwa anafanya upumbavu wa karne na kujiaibisha.
Wakati mwingine uache ujinga.
Screenshot_20200131-223650_Twitter.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom