Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Afadhali umeyaona wewe kada wetu wa ccm
Tumeshafika huko tuiombee sana nchi yetu tuvuke salama huu mwaka wa majaribu sana kwetu kama Taifa.

Rais Magufuli na Prof Kabudi wawe makini sana mwaka huu na kauli zao za mdomoni, la sivyo tutaifuta Zimbambwe iliko.

Zile kauli za kujimwambafai ziishe kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali ya Marekani imemzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingi nchini humo kutokana na kuhusika kwake kwenye uvunjifu wa Haki za Binadamu unaohusisha kunyima haki ya kuishi, uhuru na ulinzi wa watu.

Katika uongozi wake, Makonda ameonesha uonevu kwa wapinzani, kuminya uhuru wa kujieleza na kukusanyika na matendo maovu dhidi ya makundi maalum.

Marekani ina hofu kuhusu uvunjifu wa Haki za Binadamu na kupuuzwa kwa utawala wa sheria nchini Tanzania.

Kifungu namba 7031(c) kinampa uwezo Waziri wa Mambo ya nje kuweka zuio kama hili endapo mhusika amefanya ufisadi mkubwa au uvunjifu wa Haki za Binadamu. Pia kinamruhusu kuweka zuio kwa familia yake hivyo mke wa Makonda, Bi. Mary Felix Massenge amezuiwa pia.

Serikali ya Marekani inaikumbusha Serikali ya Tanzania kuheshimu utawala wa Sheria na Haki za Binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza na kukusanyika.

View attachment 1342609

Kwani Marekani wenyewe si wamezuiwa kuingia Irani kutokana na nchi yao kukiuka haki za Binadamu , haki ya kuishi Kiongozi wa Jeshi la Irani, kuingilia utawala wa nchi zingine, kulazimisha kuwa super pooowaaaa kwa kutengeneza ukituko huko China n.k.
Marekani hata Mimi mwenyewe nimegoma kwenda wasije wakanipatia Corola tu nije nayo kuwaumiza watu Wangu. Wamarekani wote wameathiliwa na akili za trumpet, Wamarekani Wanafikilia kumaliza Wasio wao n.k.
Paul Makonda kanyaga twende, wote wanaotumiwa na wazalisha corola ya China wanyooshwe
 
Kwani Marekani ni Peponi
Serikali ya Marekani imemzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingi nchini humo kutokana na kuhusika kwake kwenye uvunjifu wa Haki za Binadamu unaohusisha kunyima haki ya kuishi, uhuru na ulinzi wa watu.

Katika uongozi wake, Makonda ameonesha uonevu kwa wapinzani, kuminya uhuru wa kujieleza na kukusanyika na matendo maovu dhidi ya makundi maalum.

Marekani ina hofu kuhusu uvunjifu wa Haki za Binadamu na kupuuzwa kwa utawala wa sheria nchini Tanzania.

Kifungu namba 7031(c) kinampa uwezo Waziri wa Mambo ya nje kuweka zuio kama hili endapo mhusika amefanya ufisadi mkubwa au uvunjifu wa Haki za Binadamu. Pia kinamruhusu kuweka zuio kwa familia yake hivyo mke wa Makonda, Bi. Mary Felix Massenge amezuiwa pia.

Serikali ya Marekani inaikumbusha Serikali ya Tanzania kuheshimu utawala wa Sheria na Haki za Binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza na kukusanyika.

View attachment 1342609

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Ukizuiwa kuingia America utakosa Oxygen?

Marekan sio Peponi bana waache kujikweza

Kuna ma Billion ya Watu hawajafika America na hakuna cha maana wanakosa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa wamempa umaarufu na mtaji mkubwa wa kisiasa Makonda.
Makonda sio waziri na kazi zake hazina umuhimu wa kwenda Marekani.

Hawezi kufa kwa kushindwa kuingia Marekani, kama ana fedha ataenda kutibiwa Ulaya au India na China, anaweza kuita madaktari bingwa toka Marekani na wakamhudumia hapa hapa Tanzania.
Zaidi ya 98% ya watanzania wanakufa kabla hawajatoka nje ya Tanzania kwenda Marekani au nchi jirani za EAC.
 
Kiukweli hawa mabeberu Wamarekani ni washenzi sana!, Wanamuonea bure Makonda tena kwasababu safari za Makonda US ni safari binafsi za yale mambo ya kifamilia, kumzuia Makonda kuingia US ni ukiukwaji wa haki ya msingi ya binaadamu.

Wito kwa Rais Magufuli, toa waraka hakuna kiongozi yoyote wa serikali yako ataomba Visa kuingia US, wanataka kutudhalilisha tuu, kwani Marekani ndio nini?. Twende China!.
To hell with America!.
Let's say no to American with their filthy blood stained, stinking money except " kwa msaada wa watu wa Marekani" zikiwemo ARV.
P
Endelea kupiga kelele.

Hata wewe upo kwenye rada zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni watu wa CCM humu wasiojua kwamba si kwamba watanzania wenzao wanafurahia vikwazo dhidi ya Tanzania bali wanafurahia wanaoifedhehesha nchi yetu wanavoaibika.

Kama CCM kingekuwa ni chama cha siasa kama kilivyokuwa zamani, kingekuwa tayari kimeshachukua hatua muda mrefu sana dhidi ya watu wasioheshimu haki za binadamu wenzao wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom