Serikali ya Marekani imemzuia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingi nchini humo kutokana na kuhusika kwake kwenye uvunjifu wa Haki za Binadamu unaohusisha kunyima haki ya kuishi, uhuru na ulinzi wa watu.
Katika uongozi wake, Makonda ameonesha uonevu kwa wapinzani, kuminya uhuru wa kujieleza na kukusanyika na matendo maovu dhidi ya makundi maalum.
Marekani ina hofu kuhusu uvunjifu wa Haki za Binadamu na kupuuzwa kwa utawala wa sheria nchini Tanzania.
Kifungu namba 7031(c) kinampa uwezo Waziri wa Mambo ya nje kuweka zuio kama hili endapo mhusika amefanya ufisadi mkubwa au uvunjifu wa Haki za Binadamu. Pia kinamruhusu kuweka zuio kwa familia yake hivyo mke wa Makonda, Bi. Mary Felix Massenge amezuiwa pia.
Serikali ya Marekani inaikumbusha Serikali ya Tanzania kuheshimu utawala wa Sheria na Haki za Binadamu ikiwemo uhuru wa kujieleza na kukusanyika.
View attachment 1342609