Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Paul Makonda awa kiongozi wa kwanza kuzuiwa kuingia Marekani kwa kuwanyima watanzania HAKI YA KUISHI

Lakini Makonda si alimuomba ruhusu muheshimiwa Rais awashughulikie wanaikosoa serikali?! Kwa hiyo wanaoikosoa serikali ndio mashoga?
 
Watanzania tusitetereke. Hii ni baada ya nchi chini ya uongozi wa magufuli kusimama kidete kutetea haki yake kwenye madini. Nchi za kibeberu wamepatwa hasira na nchi yetu. Kama ni kweli wanajali haki za binadamu na sio maslahi ya kiuchumi wangeanza na mwana wa mfalme wa saudia
 
Inshort unachotuambia ni kwamba marekani hayupo interested na haki za binadamu popote duniani zaidi ya kuangalia maslahi yake, period. Ahsante kwa ufafanuzi. Sasa unatoa ushauri ganixkwa manyumbu wa Tz wanaiingizwa mkenge?
Myanmar,Yugoslavia na Bosnia kulikua na mauaji ya kutisha na uhalifu wa kivita kote huko marekani alifika kulinda maslahi ya raia ingawa hakukua na faida za kiuchumi!!

Nimeshakueleza kuwa ukiingia vitani kma upo kwa ajili ya maslahi, basi ufahamu kuna maslahi mengi zaidi ya uchumi tofauti na unavyotaka kuaminisha watu humu kuwa unavamia kisa Mafuta na dhahabu!!
 
Marekani aliingilia kupigania haki za raia wa nchi hizi
1.) IRAQ
2.) LIBYA
3.) VENEZUELA
unajua nini hizi nchi wanacho in common?, unajua nini kimewatokea? Je, na sisi wanapigania haki zetu sasa? Nini mnataka kitutokee na sisi?
Mara nyingi wanasemaga watu kama nyie mnaitumia nguvu kubwa kupinga ushoga ni mashoga pia....maana mnataka kujificha ili jamii isiwatambue.....

Hata huyo Bashite wanasema ni mdau mkubwa
 
Nimeona taarifa kwamba mkuu wetu wa mkoa ni kinara wa kukiuka haki za binadamu

Je C.I.A wamemchimba vya kutosha na wakawasilisha faili lake kwa Trump ? Kwa nini kama kweli wana ushahidi wasimpeleke ICC? Kama wao ni wanaume,tukutane ICC au watoe hati ya kumkamata

Na kama kuna mtu mnamtafuta ila mmeanzia mbali,mseme
Tuliza mshono..Marekani ni habari nyingine bwege mtozeni wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
USA pamoja na kutokuwa mwanachama wa ICC lakini ana ushawishi huko ndo maana alitishia kuacha kuwapa pesa!

Wampeleke huko badala ya hizi ngonjera!
 
Nlidhani una hoja kumbe umekaririshwa hilo swali unapewa majibu unarudia. Nimekuuliza Bosnia na Myanmar kuna faida gani ya kiuchumi au kisiasa?? Mbona umekazania Libya kana kwamba ndio nchi pekee walioingilia siasa zao.

2. Rwansa nishakujibu walimsupport Kagame ili kupambana na interhamwe,kipindi ambacho sio Tz wala mzalendo yeyote aliesaidia kule Rwanda.

3.Marekani haijawahi lazimisha watu kuingia kwenye ushoga, yenyewe mara zote ina guarantee haki za binadamu zote kuanzia haki ya kusoma hadi uhuru wa mawazo. Maana mnapoomba misaada mnasign such makubaliano, ssa kama mnataka kuua mashoga haina shida ila muende kujitoa kwenye baadhi ya declaration za human rights mlizoapa kulinda.

Mbona ni rahisi tu, sio mnawatukana hapa alafu wakiwanyima misaada mnalialia
Swali limehusu nchi tatu, Iraq, Libya, Venezuela, hizo zingine maslahi yake ni ya ki-imperilistic zaidi, maana hawana natural resources as such, nitajie nchi yenye natural resources kama hizo tatu nilizotaja au kama Tanzania amabazo marekani aliingia kutetea haki za binadamu na zikabaki salama.
 
Yaani mimi sielewi watanzania, nashauri nyimbo za kushambulia mabeberu zianze kutungwa na kuimbwa kila mahali ili uzalendo urudi
Uzalendo haulazimishwi kwa nyimbo, wala mapambio!! Huyo PAPA MOBIMBA licha ya kuvaa mishati yenye bendera, mala ilani, yupo wapi? Wote hao ni wanafiki tu, uzalendo wa wananchi kwa nchi yao ni matunda ya haki, na usawa iliyopo!! Sio kwenye unyanyasaji huu!! Kiongozi akiamua, tu imekuwa sheria, anayepigania haki za wengi anaonekana msaliti!! Usione wazungu ni wazalendo sana kwenye nchi zao ukafikiria ni suala la kuhamasishwa tu, lipo moyoni!! Wewe huduma tu za msingi, maji, afya, elimu hakuna, uniambie niwe mzalendo?!! Vipa umbele vya kiongozi mmoja ndio anavifanya vya taifa zima!!!
 
Myanmar,Yugoslavia na Bosnia kulikua na mauaji ya kutisha na uhalifu wa kivita kote huko marekani alifika kulinda maslahi ya raia ingawa hakukua na faida za kiuchumi!!

Nimeshakueleza kuwa ukiingia vitani kma upo kwa ajili ya maslahi, basi ufahamu kuna maslahi mengi zaidi ya uchumi tofauti na unavyotaka kuaminisha watu humu kuwa unavamia kisa Mafuta na dhahabu!!
Naongelea nchi zenye natural resources kama Tanzania, Iraq, Libya na Venezuela ambazo marekani aliingilia kutetea haki za binadamu na akaziacha salama. Huko kwingine anatafuta imperialistic dominance tu as a remnant ya cold war na Russia, bado wanaonyeshana umwamba kwa kuoigana vita kwenye ardhi za watu
 
Back
Top Bottom