Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiambatana na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha Lami ya Mianzini-Olemringaringa amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo kuwa anahudhuria vikao mbalimbali vya maendeleo ndani ya Mkoa wa Arusha, badala ya kuwasubiri Viongozi wa Kitaifa na kuzungumzia kero mbalimbali ndani ya Jimbo lake.
Mhe. Makonda ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kutafuta huruma ya wananchi kinyume cha taratibu, akiziita kuwa ni siasa zisizokuwa za maendeleo kwa wananchi, akiagiza kuwa ni muhimu kwa Viongozi wateule na wa kuchaguliwa kushiriki vikao vya kupanga na kuamua kuhusu maendeleo ya Mkoa wa Arusha.
Kauli ya Mhe. Makonda inafuatia maombi ya Mhe. Gambo aliyeomba kwa Waziri wa Ujenzi kujengewa barabara ya Kilombero pamoja na ufungaji wa taa kwenye barabara mbalimbali za Jiji la Arusha, masuala ambayo kulingana na Mhe. Makonda yalishajadiliwa na maamuzi kutolewa kwenye vikao mbalimbali vilivyofanyika chini ya Maagizo ya Mawaziri mbalimbali wa Kisekta ikiwemo Kikao cha mapema leo asubuhi kilichohudhuriwa na Waziri wa ujenzi Mhe. Abdallah Ulega na Waziri wa fedha Mhe. Mwigulu Nchemba.