Pre GE2025 Paul Makonda: Gambo usitake umaarufu wa kijinga, uwe unahudhuria vikao vya maendeleo Mkoa wa Arusha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Duh! kasema kabisa "Umaarufu wa kijinga". Hilo siyo tusi kwa mheshimiwa mbunge? Hivi gambo atapambania tena nafasi ya ubunge na kushinda Arusha mjini?
Gambo anastahili tusi kubwa zaidi kwa sababu na yeye alishawahi tukana mtu huko Korogwe kwa kumwambia ana degree ya chupi. Ana ushenzi mwingi tu. Gambo ni ngumu sana kuwa mbunge tena Arusha.
 
Tunahitaji kusikia upande wa Gambo pia. Huyu Bashite ana kawaida ya kutafuta umaarufu kutoka kwenye public kwa kusiliba wenzie
 
Hiki Cheo cha Mkuu wa mkoa hakitakiwi kiwepo. Gambo ni muwakilishi wa wananchi, Bashite ni muwakilishi wa Rais

Gambo hapangiwi wapi na namna gani anatakiwa ku wakilisha kero za wapiga kura wake

Bashite anafanya udikteta eti malalamiko apewe yeye, wakati hana budget. Bashite ni kigeuge Juzi alisifia wale wananchi waliomtembeza diwani kwenye maji akidai diwani hafanyi kazi., leo mbunge anafanya kazi yake ya kikatiba anaambiwa anatafuta Umaarufu wa Kijinga!! sisiem bana🙌🏿🙌🏿

Sasa kule bungeni mbunge anatafuta sifa??

Why Bashite mbona hakuna Mkuu wa mkoa mwingine yoyote anaye operate kama yeye.
 
Jiji kama Jiji.
Hakuna spana hapo Bali huyo RC hajitambui.

Ukidikiliza hoja yake Haina mashiko.Vikao anavyodai Makonda havina uwezo wa kutatua shida ya Barabara isipokuwa Viongozi wa Kitaifa

Huyo Makonda mara zote akija Rais au VP au PM Huwa anasema shida kubwa ya Arusha ni Barabara,Sasa anakuwaga hajajadili kwenye vikao?

Ni upuuzi kumkatisha mwakilishinwa Wananchi Kwa sababu za chuki binafsi.

Kama anakitaka Hilo Jimbo agombee.
 
Mfitini kivipi? Mfitini anafanya Hadharani?
Huko ni kufitinisha watendaji na public. Analeta tuhuma kwenye public kwa sababu maafisa hawawezi kujitetea kwenye public. Anachosema Bashite ni kwamba ahudhurie vikao alete hizo tuhuma katika ground ambayo muhusika anaweza kujibu na kufafanua. Ikikosa majibu na kudhibitika ndio uende public
 
Ila pia hekima ya kiungozi ni kumwambia alipokosea kiongozi mwenzako pembeni au mbele ya mamlaka yake na sio mbele ya wananch ambao hawachelewi kwenda na upepo na si hali halisi ya tukio. Kuna kitu hakipo sawa kati yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…