Uchaguzi 2020 Paul Makonda, hawezi kupita Kigamboni kura za Maoni

Uchaguzi 2020 Paul Makonda, hawezi kupita Kigamboni kura za Maoni

Kweli
Hongera zake Faustine. Mungu ni Mkubwa sana. Nilikuwa na hofu sana kuwa ataonewa. Nashkuru Mungu amesimama nae. Such a good and humble guy.
Hata mimi nilihisi hivo ila haki imefanyika
 
Naona mlima mrefu Makonda kuukwea kupitishwa Kigamboni..

Kauli za Rais zimemlenga moja kwa moja, leo tena kauli za katibu mkuu CCM zimemlenga moja kwa moja na ukuu wa mkoa utakuwa ushaota mbawa.

Bila shaka kauli zake za madharau akiwatukana watu kwamba ingawa labda nimesoma na nyie, mna vyeo kuliko mimi na wengine mmenizidi umri ila nimewazidi sana hata boss wenu anatambua, hao hao watu ndio anategemea wampitishe, wengi CCM hawampendi.

Wote walioachia nafasi zao walizoteuliwa wanataka kuonyesha kwamba uwezo wa kushinda wanao, na wakuu wao wanaonyesha wazi kuwa prove wrong.

Muda upo tusubiri.


Matokeo rasmi
----------------------------

Paul Makonda kura 122
Faustine Dungulile kura 190
UMEBETI VEMA.
 
[emoji23]
mr_misifa1_20200720_4.jpeg
 
Binafsi ninaamini Bashite hawezi kutoboa Kigamboni. Liwe jua, iwe mvua, sioni akipenya kwenye kura za maoni za CCM.

Kwa watu msiofahamu tu, viongozi wengi wa CCM Dar na wanaCCM walikuwa wanamchukia Makonda kuliko hata mpinzani. Ukuu wa mkoa ulimfanya Makonda awaone watu wengine wote ni wapuuzi, wajinga na wapumbavu.

Muda ndio huu.
Makada waamue sasa.

Yamethibitika, AMESHINDWA KUTOBOA....

Ingeshangaza sana wana CCM wasimpe nafasi Dr Faustine Ndungulile, daktari wa kweli aliyeenda shule na kusoma kwelikweli wampe anayekwea ngazi za madaraka kwa fyeti vya mtu mwingine....

Makonda ni CRIMINAL, siku nyingi alipaswa kuwa Segerea kwa kosa la "impersonating"....

Ingalau ktk hatua hii ya mchakato ndani ya chama chao, tungewashangaa sana CCM kuweka mgombea mhalifu...

Kwani, wangempitisha huyu binadamu huyu, yule mama wa CHADEMA na timu yake ya kampeni wangekuwa na kampeni rahisi sana....

Kwa Dr. Faustine Ndungulile, kampeni baina ya vyama hivi vile zitakuwa so fierce. There's no easy way by either side....
 
Hawajiongezi,mara ya kwanza walisema kigamboni lazima atabebwa,mwishowe ameshindwa,sasa hivi wanasema tena atapitishwa kwenye kura za maoni dodoma,huyu kama wangetaka kumbemba ingekuwa leo,dungule angeshafanyiwa figisu kuanzia mwanzoni,lakini wamemwacha apambane kivyake
Yani hawa jamaa ni kama wamelogwa... Huyu Makonda kawapa nini!??
 
Back
Top Bottom