Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Paul Makonda, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo
Ndugu zangu Watanzania,
Fahamu ya kuwa Ndugu Paul Makonda Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa, yule mwamba wa siasa za majukwaani na ambaye anachukuliwa kama sauti ya wanyonge na ambaye alitangaziwa Mwisho na maadui zake lakini Mungu akatangaza Mwanzo,ambaye kwake zege halilali,na ambaye anatajwa kama kijana jasiri sana katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika.
Ambaye akizungumza na kuanza ziara basi nchi yote husimama,vyombo vyote vya habari hushindana kupamba picha zake kurasa za mbele na mitandao yote hutekwa na habari zake na ambaye amekuwa kiboko ya CHADEMA anakwenda kuitikisa na Kuitetemesha mikoa kumi mfululizo kwa ziara ambayo inasubiriwa kwa hamu sana na mamilioni ya watanzania ambao walikuwa wanamsubiri kwa hamu kuwafikia huko waliko ili wamueleze kero zao kusudi azipeleke serikalini.
Sasa kama ulikuwa na shughuli yako au biashara yako unataka kuitangaza kupitia vyombo vya habari au mitandao ya kijamii,basi nakushauri usipoteze muda, ni bora usubili huyu mwamba amalize ziara yake ,maana kwa sasa anakwenda kuiteka nchi yote kimijadala na watu wote wanakwenda kutega masikio yao kusikiliza nini anazungumza na nini kinajiri katika ziara zake.
Kama wewe ni msanii na ulipanga kutoa wimbo wako basi ni bora uuweke kwanza pembeni mpaka Mheshimiwa amalize ziara zake,maana akishaingia mitaani huyu basi wimbo utakuwa ni mmoja tu ambao ni Makonda na utekelezaji wa ilani ya CCM tu.
Endeleeni kutulia Watanzania wenzangu maana najuwa mlimkumbuka sana na mlikuwa na hamu ya kumsikiliza mwamba akiunguruma kama Simba majukwaani.sasa amewasikia na anakuja kwa kishindo.
Watendaji wa serikali na wateule wa Mheshimiwa Rais andaeni majibu ya kila kitu juu ya kazi mnazofanya na kusimamia katika utekelezaji wa ilani ya CCM Katika maeneo yenu.Maana huyu mwamba huwezi kujuwa atakupiga wapi. Kumbuka huyu ni msemaji wa chama na mjumbe katika vikao vyote muhimu vya CCM. Sasa wewe lete nyodo zako huko uone kitakachokupata atakaporejea kupeleka mrejesho kwa chama juu ya aliyoyabaini mikoani huko na akina nani wanakichonganisha chama na wananchi au wanatesa wananchi au hawatoi huduma stahiki kwa wananchi au wanapuuza wananchi au hawawasikilizi wananchi.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
========For English Audience Only========
Paul Makonda, the National Secretary for Ideology and Publicity of CCM, sets off on a national tour covering ten regions. To lend a listening ear to the concerns and issues of our fellow citizens.
Makonda, is embarking on this extensive tour with the sole purpose of connecting with Tanzanians from diverse regions.
As he crisscrosses the country, Makonda aims to create an open platform for dialogue, encouraging citizens to express their grievances, share their aspirations, and contribute to the discourse on national development. it is said that this tour is not just a political spectacle; it's an opportunity for every Tanzanian to be heard.
The ten regions are poised to become the stage for Makonda's interactive sessions, where he will engage with communities, listen to their stories, and gather insights that will be crucial in shaping policies and strategies. The tour is a testament to his commitment to inclusivity, ensuring that the concerns of every Tanzanian, regardless of their location, are taken into consideration.
However, the public has criticized this act as a CCM propaganda for the upcoming elections this year and 2024 and it is not an act of service delivery to the citizens of Tanzania.