Pre GE2025 Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za Watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti

Pre GE2025 Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za Watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Na hiyo ndiyo sababu, wanafanya siasa za kuwachonganisha wananchi na watumishi wa Uma huku wao wakijiweka pembeni......Iko siku wananchi wataamka, hawataamini.
Wezi wa Nchi hii hawajawahi kuwa Watumishi wa Umma Bali Wanasiasa.Mtumishi wa Umma akikwapua ujue ameshirikoana na mwanasiasa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti, nasikia wanaangaika na mitandao...
Hana hekima, ustaarabu Hana Sifa ya kuwa kiongozii anatia Sana aibu Na kumdhalilisha mama aliyempa nafasi
 
Unajua watu hawataki kufuatilia au kusoma historia,
Bashite ni Mkuu wa Mkoa tu si Rais anafanya hivi siku akipewa madaraka ya uRais atafanya nini?...
Uko sahihi, anasema rais anatukanwa, Sasa yeye ndio analipiza rais kutukanwa kwa kutukana? Je rais ametukanwa na mtu mwenye nafasi rasmi ya kiutawala, au wahuni wa mitandaoni? Halafu anamtaja rais ili ionekane ana uchungu sana na rais, kumbe ni utetezi wa kichawa.

Huyo dogo alipata madaraka atatawala kama alivyotawala Magufuli. Na hata hiki anachokifanya ni carbon copy ya alichokuwa anakifanya Magufuli.
 
Habari JF.
This goes to Makonda.

Tukicheka na hivi vijumuia vinavyojiita vya wanawake vitatusumbua sana mpaka kwenye ndoa zetu.

Kama kweLI wapo serious waanze kujikemea wenyewe wanavyojidharirirsha kwenye miziki kwa kucheza uchi na kuruhusu kushikwa shikwa ovyo.

Wengi wao wanavaa nusu uchi mtaani na wanaleta tabu sana kwa vijana, lakini CHATANDA hakemei.

Zuchu katusi kule Zenji lakini hatukusikia wakemee.


Kuna wengine wanajirekodi picha za ngono na wanazirusha mitandaoni lakini CHATANDA yupo kimya. hakemei.

CCM kutetea wezi na wazembe imekuwa kama huruka yao, that's why wanamshambulia Makonda.

Makonda 'piga spana' hao mpaka watanyooka tu.

#HAKUNAKUCHEKANAWAZEMBE
1716813172638.png
 
Kwa kweli Makonda ana kibri na maneno machafu sana. Na hiki ndicho ambacho watu wanalalamikia.

Hata kama anajiona mchapakazi basi huo uchapakazi wake usiwe chanzo cha kudhalilisha na kubagaza utu wa watu wengine, regaardless of their status in the community or level in civil service...
Taja maneno machafu angalau mawili na sheria aliyovunja ya utumishi wa umma ili twende pamoja, ukishindwa wewe ni idiot
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesema anawashangaa wanaojitokeza kusema anawadhalilisha Watumishi baada ya yeye kuwakosoa Wala rushwa na Wazembe wakati Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan alidhalilishwa siku kadhaa zilizopita na Watu hao wakiwemo Wanawake wenzake walikaa kimya na kumuacha yeye Makonda akisimama kumtetea Rais.

Akiongea leo May 27,2024 wakati akianza ziara yake Wilayani Monduli Mkoani Arusha, Makonda amesema “Wale mnaotoatoa kauli muendelee inanisaidia kwakweli, inanisaidia kufanya kazi kwa morali mkubwa zaidi na siku moja nilisema Umoja wa Waovu, Wala rushwa na Wazembe ni mkubwa sana, wewe ukitaka kujua kama upo mguse Mvivu mmoja Wavivu wote unaona wanajitokeza, au mguse Mla rushwa mmoja, Wala rushwa wote wanajitokeza”

“Nawaambia tena nitawapiga spana na mnapojitokeza tunapata nafasi ya kujua aah kumbe nae huyu yumo, alidhalilishwa hapa Rais wetu, Mwenyekiti wa Chama, Mwanadiplomasia namba moja, Mama mwenye Familia, katukanwa asubuhi mpaka asubuhi sikusikia kauli ya Mtu yoyote halafu Wanaume sisi ndio tulijitokeza kumpigania yule Mama, leo Mzembe mmoja, Mla rushwa mmoja, Mvivu mmoja mnapigapiga kelele huko eboo, twende kwenye kazi”

My Take
Samia anatumika kama kinga ya Makonda kudhalilisha wengine?
 
Hivi Rais aliwahi kutukanwa matusi ya nguoni au anamtaja Rais mara kwa mara li kutafuta huruma zake?

Kama kuna matusi ambayo Rais aliwahi kutukanwa naomba mtu anitag tafadhali.

Back to the point. Huyu jamaa inaonekana ni mgumu sana wa kuelewa na mwepesi wa kusahau. Hakuna mtu aliyemzuia kupambana na wavivu na wala rushwa.

Kinacholalamikiwa na watanzania wapenda ustaarabu ni udhalilishaji wa watumishi wa umma katika harakati zake hizo anazoendelea nazo. I think this guy is missing a point somewhere and sometimes.

Kama angekuwa mtu muelewa na mwenye akili timilifu, angegundua ni wapi alipojikwaa na kuomba radhi badala ya kuendelea kushupaza shingo na kumvua nguo aliyemteua kushika wadhifa huo. Mtu huyu hana washauri bali amezungukwa na wahuni kama yeye
Kama kuna mtu kadhalilishwa sheria ziko wazi mahakama ziko huru, fungueni jalada la udhalilishaji dhidi yake, kama hamuwezi nyie ni wachawi tu,

Mmemuita mwizi, jambazi dhulmati, sijawahi ona kesi hata mooja dhidi yake leo ni miaka minne, haumoni ya kwamba wewe na wenzako ni mapunguani?

UWT,LHRC na wewe pia saidieni huyo mdhalilishwaji kufungua jalada, pathetic!
 
Habari JF.
This goes to Makonda.

Tukicheka na hivi vijumuia vinavyojiita vya wanawake vitatusumbua sana mpaka kwenye ndoa zetu.

Kama kweLI wapo serious waanze kujikemea wenyewe wanavyojidharirirsha kwenye miziki kwa kucheza uchi na kuruhusu kushikwa shikwa ovyo.

Wengi wao wanavaa nusu uchi mtaani na wanaleta tabu sana kwa vijana, lakini CHATANDA hakemei.

Zuchu katusi kule Zenji lakini hatukusikia wakemee.


Kuna wengine wanajirekodi picha za ngono na wanazirusha mitandaoni lakini CHATANDA yupo kimya. hakemei.

CCM kutetea wezi na wazembe imekuwa kama huruka yao, that's why wanamshambulia Makonda.

Makonda 'piga spana' hao mpaka watanyooka tu.

#HAKUNAKUCHEKANAWAZEMBE
View attachment 3000823
Unamlinganisha Zuchu na RC !
 
Back
Top Bottom