Pre GE2025 Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za Watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti

Pre GE2025 Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za Watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama kuna mtu kadhalilishwa sheria ziko wazi mahakama ziko huru, fungueni jalada la udhalilishaji dhidi yake, kama hamuwezi nyie ni wachawi tu,

Mmemuita mwizi, jambazi dhulmati, sijawahi ona kesi hata mooja dhidi yake leo ni miaka minne, haumoni ya kwamba wewe na wenzako ni mapunguani?

UWT,LHRC na wewe pia saidieni huyo mdhalilishwaji kufungua jalada, pathetic!
Ndio. SIsi sote ni MAPUNGUANI.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesema anawashangaa wanaojitokeza kusema anawadhalilisha Watumishi baada ya yeye kuwakosoa Wala rushwa na Wazembe wakati Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa...
Wanaume wa bongo ni vyema tujikiteni kufanya kazi habari za kujadili mambo ya udaku tuwaachie wahudumu wa saloon!
 
Alishasema hahitaji sifa anachohitaji watendaji wafanyie kazi kazi ndizo zitaamua

Sehemu zingine ananyamazisha Hadi watendaji wanaotamka Kila dakika mheshimiwa mkuu wa mkoa anasema we niite hata makonda tu Lete ripoti ya Mradi.Hayo ya mheshimiwa kunipamba pamba achana nayo leta ripoti
Kwani ni lazima aonyeshe uchapa kazi mbele ya makamera? Tuchukulie mganga mkuu wa Hospital anaitisha madoctor wake watoe taarifa mbele ya macamera Ili ionekane ni bonge la mchapakazi, katika mazingira hayo utaona ni uchapa kazi au ni kiki?
 
Kama kuna mtu kadhalilishwa sheria ziko wazi mahakama ziko huru, fungueni jalada la udhalilishaji dhidi yake, kama hamuwezi nyie ni wachawi tu,

Mmemuita mwizi, jambazi dhulmati, sijawahi ona kesi hata mooja dhidi yake leo ni miaka minne, haumoni ya kwamba wewe na wenzako ni mapunguani?

UWT,LHRC na wewe pia saidieni huyo mdhalilishwaji kufungua jalada, pathetic!
Akashitakiwe kwenye mahakama zipi, hizi zinazopigiwa simu Moja?
 
Kwani ni lazima aonyeshe uchapa kazi mbele ya makamera? Tuchukulie mganga mkuu wa Hospital anaitisha madoctor wake watoe taarifa mbele ya macamera Ili ionekane ni bonge la mchapakazi, katika mazingira hayo utaona ni uchapa kazi au ni kiki?
Haujawahi ona madaktari wakiweka kambi za wazi za kutoa damu,au tiba au kiliniki nk za Bure?
 
Kwenye hili genge la CCM, kuliko uwe mkweli, utumikie watu kwa dhati ya moyo bora uwe mwizi na mwongo otherwise hutoboi. Shame
 
Kinachodaiwa ni kuheshimiana maana hakuna binadamu perfect!! Mbona wengine wameibaga hadi majina na wanadunda serikalini
 
Ila nyie WAPUMBAVU mnateseka sana,utafikiri mmekalia kitu chenye ncha kali.
 
Huyo mama aliyetukanwa hadharani na Makonda ni mwakilishi wa Mange Kimambi? Ndiye aliyemtuma Mange kufanya alichofanya?
Hajamtukana, amemweleza ukweli tu. Watanzania munapenda maneno kuliko kazi. Maneno haya kuliko kazi, ndio yametawala ofisi za serikali. Kwa lugha nyingine tunayahita majungu.

Amos Makalla yupo wapi kwenye uenezi.? Hawezi kaz, anaweza maneno na majungu tu. Hata huyu Chatanda anaweza maneno na majungu tu.

Si rahisi Tanzania kuendelea kwa kuwa kazi ya mtu inapimwa kwa uwezo wa majungu na sio kaz zake.

Hapo ndipo utaona wazi CCM imegawanyika kabisa. Makonda anaogopeka kwa kazi. Timu Msoga, haiwezi kazi ni majungu tupu.
Huyu Chatanda anamshambulia vipi, mwanaccm, aliyeteuliwa na mkuu wa nchi? Kwann usimpigie simu mkaongea? Au ndio kutumwa na Kinana? Hii timu Msoga inategemea Makala aeneze CCM, vip wakati hawezi kazi?
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amesema anawashangaa wanaojitokeza kusema anawadhalilisha Watumishi baada ya yeye kuwakosoa Wala rushwa na Wazembe wakati Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan alidhalilishwa siku kadhaa zilizopita na Watu hao wakiwemo Wanawake wenzake walikaa kimya na kumuacha yeye Makonda akisimama kumtetea Rais.

Akiongea leo May 27,2024 wakati akianza ziara yake Wilayani Monduli Mkoani Arusha, Makonda amesema “Wale mnaotoatoa kauli muendelee inanisaidia kwakweli, inanisaidia kufanya kazi kwa morali mkubwa zaidi na siku moja nilisema Umoja wa Waovu, Wala rushwa na Wazembe ni mkubwa sana, wewe ukitaka kujua kama upo mguse Mvivu mmoja Wavivu wote unaona wanajitokeza, au mguse Mla rushwa mmoja, Wala rushwa wote wanajitokeza”

“Nawaambia tena nitawapiga spana na mnapojitokeza tunapata nafasi ya kujua aah kumbe nae huyu yumo, alidhalilishwa hapa Rais wetu, Mwenyekiti wa Chama, Mwanadiplomasia namba moja, Mama mwenye Familia, katukanwa asubuhi mpaka asubuhi sikusikia kauli ya Mtu yoyote halafu Wanaume sisi ndio tulijitokeza kumpigania yule Mama, leo Mzembe mmoja, Mla rushwa mmoja, Mvivu mmoja mnapigapiga kelele huko eboo, twende kwenye kazi”

My Take
Samia anatumika kama kinga ya Makonda kudhalilisha wengine?
Je ni afya kuendeleza malumbano na ubabe. Je Ukiwa myenyekevu ni ujinga?
 
Back
Top Bottom