Paul Makonda na William Malecela waburuzwa kizimbani kwa tuhuma za kudhulumu gari

Paul Makonda na William Malecela waburuzwa kizimbani kwa tuhuma za kudhulumu gari

Hii ndio taarifa mpya na ya kusisimua kutoka kwenye lile gazeti makini la Raia Mwema .

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa maendeleo ya Kesi hii mpya .

---

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na William Malecela maarufu Lemutuz wamefunguliwa kesi mahakamani kwa tuhuma za uporaji wa gari aina ya Range Rover.

Makonda na Lemutuz wamefunguliwa kesi hiyo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mfanyabiashara Patrick Christopher Kamwelwe ambaye katika madai yake anataka alipwe fidia ya zaidi ya TZS milioni 240 ambazo ni gharama za kodi na thamani ya gari hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Wakili wa mfanyabiashara huyo, Kung’e Wabeya amesema tayari mahakama hiyo imetoa taarifa kwa wadaiwa kuhusu kesi hiyo na kuwataka wawasilishe mahakamani utetezi wao wa maandishi ndani ya siku 21 tangu kupokea taarifa hiyo.

Ameongeza kuwa endapo wadaiwa watashindwa kuwasilisha mahakamani utetezi wao ndani ya muda huo, mahakama itaweza kutoa hukumu dhidi yao.

Wabeya amesema kesi hiyo ya madai namba 234 ya mwaka 2022 imepangwa kutajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Oktoba 13, 2022 saa 7 mchana.


View attachment 2379487
huenda ni ukweli au anaonewa tu.huyo mfanyabiashara siku zote hizo alikuwa wapi kwenda mahakamani?nina imani mengi tutayasikia ktk kesi hiyo.inawezeka pia huyo mfanyabiashara aliitoa kama rushwa na kama ndivyo basi naye apandishwe mahakamani kujua mazingira halisi kwa namna gani hilo gari liliporwa.
 
Hakuna mtu mnafiki hapa duniani kama huyo lemutuz... kwenye utawala uliopita aliwapotezea kabisa kina Ridhiwani ila baada ya utawala ule mapema kabisa akawakana JPM & Makonda kwa kuandika waraka mrefu huko Instagram. Yule mzee akiwa rafiki yako kuwa makini sana.
Mzee wa fursa yule..
 
Jamani mdai si angechukua tu gari na amsamehe?
Jee unajua ni lini hilo gari lilitekwa? Jee unajua hili gari liko katika hali gani hivi sasa? Jen unajua ni maili ngapi hilo gari limeshasafiri hadi sasa? Unadhani thamani ya gari hii muda huo ilipotekwa hadi leo haikushuka kutokan ana ukongwe wake?
 
hatma ya kesi hii ipo mikononi kwa DPP. kumbukeni DPP anateuliwa na Rais ambaye ndiye mwenyekiti wa chama chetu .. kwa hiyo hili suala la kama Makonda ajibu ama asijibu tuhuma limo ndani ya chama chetu, wengine mnajichosha.
Na mimi pia niko chama chetu chenye maadili.
Chama hakiruhusu uporaji na wizi.
 
Hakuna mtu mnafiki hapa duniani kama huyo lemutuz... kwenye utawala uliopita aliwapotezea kabisa kina Ridhiwani ila baada ya utawala ule mapema kabisa akawakana JPM & Makonda kwa kuandika waraka mrefu huko Instagram. Yule mzee akiwa rafiki yako kuwa makini sana.
Success has many fathers, failure is an orphan!

Unakwenda na wenye nafasi na mafanikio, waliofeli watakusaidia nini? Mjini mipango
 
Ongeza na hili hapa

1665132963500.png
 
Jamani watamuua Lemutuz, libabu la watu kwa Presha. limechoka alafu analetewa makes mengine. Walimwengu siyo wema kabisa

You know, I am super humbled sana.
 
Back
Top Bottom