Paul Makonda na William Malecela waburuzwa kizimbani kwa tuhuma za kudhulumu gari

Paul Makonda na William Malecela waburuzwa kizimbani kwa tuhuma za kudhulumu gari

Huyu lemutuz si aliwahi andika andiko lake kuwa makonda enzi ya mwenda zake aliwatenga washkaji zake na akiwemo na yeye hiib dili lini?
 
DAB alipora magari na nyumba/viwanja vya matajiri wengi na kuwabambikizia kesi za kuuza "BWIMBWI".
 
We have a root problem in Tanganyika that is CCM [emoji1787][emoji1787][emoji1787] The same level of thinking that created problems,is the one that try to find the solutions to the problems they have created [emoji137][emoji137][emoji137]
View attachment 2380281
 
DAB ni mwizi, mporaji wa mali za watu. Akishirikiana na mwenda zake wamesababisha makovu makubwa sana kwa watu wengi. Nawashangaa mnaosema eti huyu anafaa kuwa Rais ajaye.
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na William Malecela maarufu Lemutuz wamefunguliwa kesi mahakamani kwa tuhuma za uporaji wa gari aina ya Range Rover.

Makonda na Lemutuz wamefunguliwa kesi hiyo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na mfanyabiashara Patrick Christopher Kamwelwe ambaye katika madai yake anataka alipwe fidia ya zaidi ya TZS milioni 240 ambazo ni gharama za kodi na thamani ya gari hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Wakili wa mfanyabiashara huyo, Kung’e Wabeya amesema tayari mahakama hiyo imetoa taarifa kwa wadaiwa kuhusu kesi hiyo na kuwataka wawasilishe mahakamani utetezi wao wa maandishi ndani ya siku 21 tangu kupokea taarifa hiyo.

Ameongeza kuwa endapo wadaiwa watashindwa kuwasilisha mahakamani utetezi wao ndani ya muda huo, mahakama itaweza kutoa hukumu dhidi yao.

Wabeya amesema kesi hiyo ya madai namba 234 ya mwaka 2022 imepangwa kutajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Oktoba 13, 2022 saa 7 mchana.


View attachment 2379487
Maisha hubadirika au sio
 
Back
Top Bottom