Makonda anateuliwa kwa lazima fulani lakini huwa mambo hayo yana mwisho wake.
Ana makosa flani anafanya kila wakati tangu alipokuwa RC Dar na ameendelea kuyafanya siku zote.
Kitendo cha kuingia Arusha na msafara mrefu wa magari ndio kosa lake la kuanzia katika ajira yake mpya.
Tayari bila weledi wowote ameshatoa oda uhamiaji kuharakisha passport za watu wa Arusha kutoka siku 14 hadi siku 3!
Makonda baada ya miezi 4 atakuwa amevuruga utalii Arusha na kuharibu diplomasia ya Arusha.
Mwisho Makonda ataondolewa Arusha na anaweza akajikuta tena akirudi kulialia na kuomba “manabii”wamwombee.
Makonda ni mtu ambaye yupo "optimistic" sana kwa kile ambacho anakiamini, lakini anakosa "the right tactical skills" ya kiuongozi. Akiwa kama kiongozi wa juu wa mkoa kupitia katika cheo hicho cha ukamishna wa mkoa, anapaswa kutumia zaidi "abstract & administrative skills" kuliko zile za "technical" ili matokeo ya maamuzi yake yaonekane kupitia timu ya wasaidizi wake.
Hivi vitu vya kujionyesha kama vile misafara mirefu, na kupiga mkwara hadharani wasaidizi wake ni dalili za kutaka kujenga vitisho kwao ili kuogopwa. Ukikabidhiwa jukumu kama hilo la ukamishna wa mkoa, kitu cha kwanza ni kujipa muda wa kutosha ili kusoma mazingira ya kiutendaji kuliko kuanza kutoa matamko ambayo mengine yanakosa uhalisia wowote ule.
Haiwezekani, day 1 tu, unakuja na kuanza kuzungumzia masuala ya muonekano mpya wa Jiji la Arusha na miundombinu yake, bila hata kukutana wa wahusika na kuangalia uwezekano wa kufanya hivyo kutokana na bajeti iliyotengwa. Kamishna aliyeondoka John Mongella amekuwa ni bosi wake ki chama, kwa kuwa hayo makeke yake anayoyaropoka hadharani ni kama vile kutaka kuuambia umma aliyepita ni mtu legelege na alikosa ubunifu akiwa katika ofisi hiyo.
Ameingia kwa mguu mbaya ili kujijengea sifa yeye binafsi bila ya kutaka kujenga "team work spirit" kwanza. Asipoangalia atajikuta yupo peke yake na kila anachokifanya anawakwaza wenzake. Aangalie jinsi makamishna wenzake wanavyotenda katika zama hizi za utawala wa SSH kwa kuwa hizi si tena zile za JPM.
La sivyo jombii itakula kwake. Arusha pana siasa za kimafia, na hazifanani kabisa na zile za kipwani. Sikio lisikilizalo kamwe haliwezi kukatwa kichwani. Shauri zake!