Ngurukia
JF-Expert Member
- Feb 25, 2023
- 4,407
- 16,942
Kwa wakati ni busara kukaa kimya.Wakuu,
Inaonekana leo Makonda ameamua kusema yote ya rohoni
Akiwa anaongea rasmi na wanahabari, Makonda amesema kuwa clip inayomuonesha akiwa anaingia na bunduki Clouds ilitumika vibaya kupotosha na kwamba Clouds wamemtumia sana yeye kuliko yeye alivyowatumia.
"Hakuna kituo chochote kilichowahi kuvamiwa chini ya uongozi wangu. Clouds ilikuwa ni familia yangu. Walinzi niliokuwa nao wa nyumbani kwangu, ndo walinzi ambao hata Ruge mwenyewe akikwama ndo walikuwa wanawapigia simu"
"Pale tulikuwa tunaenda kufanya editing, tunatoka tunarudi. Sasa swali kubwa ambalo natamani wandishi wa habari mngefanyia kazi. Moja, mbona hamjawahi kudai clip za mule ndani nilienda kufanya nini? Kwanini mliamini tu ya kwamba mtu ameonekana kuingia pale mlangoni alafu ndo ikawa chanzo cha uvamizi?
"Na cha pili hata yule mlinzi mwenyewe aliyekuwepo, kabonyeza ile button comfortable kabisa. Nilikuwa naenda mchana nilikuwa naenda usiku so many times. Ingekuwa ni investigation proper, wangeomba okay fine, hivi kwa mwezi wote mzima Makonda alikuja mara ngapi hapa?"
" Ni chombo ambacho hakijawahi kuvamiwa na mimi. Infact mimi nimetumika zaidi na Clouds, kuliko nilivyoitumia Clouds. Can you imagine ilikuwa imefika hatua wanaitwa na TCRA mimi na-show up, Ruge anapiga simu Brother eeh jamaa wamekuja TCRA, tuna kimeo hapa. Wananiambia niko wapi nawaambia tulia nakuja"
Kwahiyo anakiri kutumia madaraka yake vibaya kuzuia mamlaka nyingine kama TCRA kufanya kazi zao.