Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Eti anapendwa?. Si ni huyu Makonda alipigwa Chini kwenye Ubunge wa Kigamboni akapotea kwenye ramani.
 
Makonda mfano avae viatu vya Lisu awe upinzani kitambo angekuwa ameunga mkono juhudi kukimbia Ligi kuu. Na Lisu angekuwa upande wa serikali ccm kitambo hata kabla ya Magu angekuwa presideeerrrr
 
Nilisemaga kichaa pekee ndo atashindwa kumuelewa JPM kipindi kile anatawala wengi wakabisha,Alivyo-itangulia haki wakaanza kumkumbuka.
Sasa nasema tena kichaa pekee ndo atashindwa kumuelewa PCM.
Magufuli amepata kiki kutokana aliyeingia kuwa boya. Ila uboya wa aliyepo haumfanyi Magufuli kuwa Bora. Halafu msipende kulazimisha watu kwenye maamuzi yenu.
 
Ukishakuwa rafiki wa wazungu ww siyo mzalendo tena. Nitajie kiongozi mzalendo ambaye ana urafiki na mabeberu?
Wewe naye?. Mumpige Lissu risasi halafu aende ubelgiji kwa matibabu zaidi , halafu wewe kumbe mwenye roho mbaya unaleta stori za mababeru. Huyo Magufuli mbona alikuwa anakopa kwa mabeberu?.
 
Ukishakuwa rafiki wa wazungu ww siyo mzalendo tena. Nitajie kiongozi mzalendo ambaye ana urafiki na mabeberu?
Huyo Bashite mtoto kampatia marekani kwenye surrogate. Unaijua Hilo?. Tatizo mnaongea bila utafiti.
 
Safi Sana umempa jibu la maana huyo mjinga.
 
Alifanya biashara nao ila hakuwanyenyekea kama ilivyo marais wengine
Aliwanyeyekea ndio maana kila mwezi alikuwa analipa Deni la bilioni mia Saba za kitanzania. Acha mchezo wewe. Eti alikuwa hawanyenyekei wakati wamemfuka kifaa Cha pacemaker moyoni.
 
Wewe mleta mada una matatizo umeona ukae huko uje ulete Uzi wa kumlinganisha Makonda na Lissu. Kwanza Makonda Hana time na Lissu maana wote wanawasulubu CCM , Sasa wewe mnafiki kwa kulijua Hilo umekuja kuleta comparison
 
Kwa wanaoumia mioyo yao kuona Makonda anaupiga mwingi, sageni chupa kunyweni.
Makonda ni mtendaji. Siasa za uongo, unafiki kwake hizo hakuna. Siasa za kuabudu aliyemtua hakuna. Anajua JD yake hadi anapitiliza. Kwa kimombo tunasema anaenda extra miles.

Alisema kwa wanaomuombea atenguliwe nafasi hiyo ya mkuu wa mkoa, yeye kajibu hata akiwa mkuu wa mkoa kwa siku moja inatosha.
Hiyo ni kauli ya kishijaa sana. Anaamini hata siku moja itatoa matokea chanya.

Namalizia kwa kusema

Amtumainiye BWANA ni kama Mlima Sayuni usiotikisika milele.

Kitenguliwa siyo jambo la kushangaza.

Piga kazi Makonda chali wa Yesu.
 
Ccm hawawezi kumchagua paka wasiemweza kumfunga keñgele kama ilivyokuwa kwa magufuli.watamçhagua mtu ambae wanaweza kumzibiti ili wasije letewa madhara kama magu.ña walijuta kumchagua magu
 
Nasemaje nawachukia CCM ila mwamba ni jembe
Hana kujipendekeza pendekeza kama machawa wengine.

Anajikubali kiasi kwamba hata raia wanaona wapo mikono salama mwa makonda.

Mtu ukiwa mzembe mzembe huwezi kulinda raia wako na hutopata attention ya wananchi wako.
 
Simfananishi Lisu na Makonda ila ukweli kila mtu anajua Makonda ni RC wa Arusha, hivi hata RC wa Mkoa wangu namjua kwa sura na sio jina na mienendo yake kama ilivyo kwa Arusha. Unaweza sema Tanzania kuna Mkuu wa Mkoa mmoja tu,
 
kijana anafanya kazi nzuri sana na mambo makubwa ya kufuta machozi ya wanyonge n.k

atafika mbali mchana kweupe kila mtu akimtazama 🐒
 
Aliwanyeyekea ndio maana kila mwezi alikuwa analipa Deni la bilioni mia Saba za kitanzania. Acha mchezo wewe. Eti alikuwa hawanyenyekei wakati wamemfuka kifaa Cha pacemaker moyoni.

..nadhani barrick walimhonga Jpm.

..mkataba aliosaini nao hauendani na mikwara na makelele aliyokuwa akipiga.

..mwisho wa siku aliruhusu makinikia yasafirishwe.

..na zaidi Jpm alimpa ubunge Deo Mwanyika aliyepata kuwa mtendaji wa ngazi za wa barrick / acacia hapa Tanzania.
 
Agombee Jimbo gani?
 
Makonda na Lisu ni watu wawili tofauti. Makonda ni kiongozi mzuri na mchapakazi mzuri na Lisu ni mwanaharakati mzuri na mjenga hoja mzuri ambaye ana uwezo mkubwa wa kuitetea na ikaaminika hata iwe ya uongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…