Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Acheni kufananisha upuuzi wenu na vitu vya maana
Eti arusha iwe Geneva labda iwe jenista
Kuna wengine Tabora (M) iwe Toronto?
 
Chini ya uongozi wa Comrade Dr Makonda. Jiji la Arusha litaizidi Geneva kwa miundombinu, huduma za jamii na kupokea idadi kubwa ya watalii
Kweli mtaji wa ccm ni ujinga. Makonda alibadilisha nini Dar? Makonda anapanga bajeti ya miundombinu huko wizara ya ujenzi? Makonda anawezaje kuongeza mapato ya halmashauri? Wazungu wanaokuja kutalii wanajua RC wa Arusha ni nani?
 
Hatutaki Makonda awe controlled na Gambo. Hata kama ni marafiki...Gambo atamdanganya Ili kuficha makosa aliyoyafanya alipokuwa RC..mfano issue ya stendi ndogo, Gambo husimama mbele ya viongozi na kusema uwongo huku akijua eneo lile ni la serikali na limehodhiwa na wachache wenye connection.

Wale wafanyabiashara kwenye vile vibanda ndio wanateseka na hakuna wa kuwatetea, hawana connection na wakubwa wananyang'anywa mali zao kila siku...wananchi wanateseka kwenye nchi Yao wenyewe...hao walionunua Mali ya serikali huchanga fedha Kila mara kumlipia Gambo....hua ni za nini??
 
Salaam wakuu. Nimeona vema kumpongeza Mheshimiwa Makonda kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatetea wanyonge.

Hakika si kazi ndogo. Tunapoona watu wamejaa kwenye mikutano yake hii inamaanisha wanaimani naye. Na hakika anaweza kutokana na uthubutu alionao.

Mkuu hata kama tumekutafsiri vibaya kutokana na ubinadamu wetu, lakini wewe endelea kufanya kile ambacho Mungu anakuwezesha.

Barikiwa sana.
 
Gambo sio wa kumuamini yule,ni muongo muongo
Makonda afanye kazi aachane nae atamchelewesha
 
Makonda ni propaganda machine!
Populist! Attention seeker. Bingwa la kubwabwaja!
Wadanganyika wengi wanapenda ulaghai!
 
Kama nikweli huo nao ni unyang'anyi na utapeli
 
Muda hauongopi. Tutaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…