Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Baadhi y watanzania kama hili lianzisha mada ni empty set kabisa. Arusha ina nini cha ajabu. Au uharifu unaofanywa na watoto wa mitaani waliokosa malezi bora ya wazazi wao ndio sifa njema kwao. Hao vibaka ndio wa kumsumbua makonda kweli. Ngoja tuone.
Empty Set ni Mamaako Mzazi na siyo Mimi tafadhali.
 
Tatizo hata huko Ubalozi anaweza Kufika na kumpa waziri wa Nchi husika wiki Moja awe ametatua matatizo yote.
 
Kwa kuwa wewe umejinasibu kama rais wa Arusha, basi uzingatie yafuatayo la sivyo hutakuwa na maana isipokuwa a political empty barrel.

Kwanza hakikisha uwanja mpya wa mpira wa kisasa wa Olmotonyi unajengwa mapema kuanzia sasa la sivyo tutashindwa ku-host Afcon in June-Julay 2027.

Pili uhakikishe barabara ya njia sita kutoka Arusha hadi Moshi inakamilika mradi huu ulisimamishwa kuanzia 2015.

Tengeneza metropolitan ya Arusha-Moshi iwe tourist hub ya Afrika. Hii natural confluence iliyopo katikati ya miji hii miwili haipo pengine Afrika na ni potential kubwa ajabu, take that advantage.

Tatu hakikisha kituo kipya cha mikutano cha Kilimanjaro International Convention Centre kinajengwa mapema na kwa ubora wa hali ya juu.

Makonda weka express train Moshi-Arusha, ni takriban 75km kwani watu wengi sana tunataka kuishi Moshi na kufanya kazi Arusha au kinyume. Tunaweza kuiita treni ya Makonda kama itafanikiwa. Unaonaje?

Makonda hakikisha ujenzi wa stendi mpya na ya kisasa Arusha unafanyika vizuri na kukamilika haraka, iwe ya kipekee na sio lazima iwe na maghorofa yasiyotumika kama stendi ya JPM Mbezi.

Watu wanataka kuona Arusha ya kweli ya kimataifa; hakikisha taasisi za Africa Mashariki na zile za Afrika nzima zilizopo Arusha zinapatiwa ardhi ya kutosha, nyumba nzuri na huduma nyingine nzuri kwa ma-experts wanaokuja kuisha na kufanya kazi Arusha.

Kuwa kwako mkuu wa mkoa wa Arusha hakutakuwa na maana yoyote ile kama hutafanya mipango miji katika jiji la Arusha lililokaa hovyo na lenye vichochoro na makazi yasiyo rasmi kila kona. Jiji la Arusha linahitaji master plan mpya. Maeneo kama Unga Limited na Kwa Muorombo ni aibu kubwa kwa hiyo Geneva of Africa, fumua na suka upya haya maeneo kama wewe kweli ni kiongozi mahiri kama unavyojinasibu.

Makonda hakikisha ile miradi ya nyumba za kisasa na satelaite towns za Arusha zilizoanzishwa na Nehemia Mseshu na kuuwawa na Magufuli zinafufuliwa. Makazi ya Arusha bado ni duni kwa watu wa kimataifa na matajiri wa maeneo hayo ambao wangependa kuisha kama Ulaya.

Makonda uongozi wako Arusha utahesabika sio lolote wala chochote kama hutafanya kazi kuhakikisha utalii hapa Arusha unafanywa professionally, kuna vikampuni vingi vya hovyo vinavyoharibu taswira ya utalii Tanzania, hakikisha kunakuwa na uhakiki wa ubora wa wale wote wanaohusika na tour guiding, ma-tour guide wengi ni wahuni, walevi na vilaza wakubwa na mara nyingi huishia kuwa-harrass watalii.

Hakikisha Arusha inakuwa Geneva of Africa ya kweli. Panua ukubwa wa jiji hadi kukaribia KIA au kuunganisha kabisa na Moshi na kutengeneza a larger metropolitan area. Ongeza barabara za hali ya juu za lami na barabara hizi zipite maeneo yenye makazi ya watu wengi kama Usa River nk. Makonda hakikisha Arusha inakuwa na hoteli za hali ya juu za kimataifa, hakikisha kunakuwa na open spaces (parks) kila baada ya nusu kilometa.

Acha majigambo, fanya hayo hapo juu utaonekana kiongozi kwa standard za Arusha. Pia jua kuwa Arusha ni pagumu zaidi ya Dar, unaweza kuaibishwa na ma-chapaa au ma-chalii wadogo tu hapa mjini.
 
Tatizo la mkoa wa Arusha ni kuwa hata kwenye CCM kuna mamluki wa CHADEMA kibao. Kuna watu walikuwa supporters wa CHADEMA leo hii ni viongozi wa CCM huko Arusha. Lema kutamba ina mambo mengi sana nyuma yake. Tena bora Arusha mjini... huko Karatu ndo balaa. Wale wairaqw wakiamua lao hakuna kitu utawaambia. Wameru nao sio poa kabisa. Monduli pekee ndo kuna afadhali. Aende kwa tahadhari. Chama chetu cha CCM kinahitaji mpango mkakati wa kisayansi sana ili kwenda sawa na siasa za mkoa wa Arusha.
 
Unabwabwaja.

Hiyo budget, labda nchi iache kushughulika na mambo mengine yote. Pesa zote zielekezwe Arusha.

Makonda fanya yaliyo ndani ya uwezo wako.
 
Hii ni kazi ya Mkuu wa Mkoa kweli? Kujenga barabara ya njia sita?! Kweli?!
Huyo bwana anadai kuwa anaweza kuwa kiongozi wa aina yoyote ile basi embu atufanyie hayo basi tuone kweli Makonda ni kiongozi na rais wa Arusha kama anavyosema.
 
Hapo kwa waendesha utalii ndipo nilipokuona kumbe huna kitu cha kushikika cha kumshauri Mh Makonda.
Utalii huu umefikishwa hapo na hao unaowadharau..Mh Makonda awafikie hawa Tour Guides,achote hazina ambayo ikilindwa,nchi itapaa!
 
Hapo kwa waendesha utalii ndipo nilipokuona kumbe huna kitu cha kushikika cha kumshauri Mh Makonda.
Utalii huu umefikishwa hapo na hao unaowadharau..Mh Makonda awafikie hawa Tour Guides,achote hazina ambayo ikilindwa,nchi itapaa!
Hayo ni mepesi, hata Jokate anaweza.
 
Mwenzio anaangalia miradi ya kumpa teni pasenti na wafanyabiashara wa kuwatisha wampe hela, na wa kujipendekeza pia wampe hela, usidanganywe na sanaa za majukwaani ukadhani ndio ukweli
 
Back
Top Bottom