Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kwa kuwa wewe umejinasibu kama rais wa Arusha, basi uzingatie yafuatayo la sivyo hutakuwa na maana isipokuwa a political empty barrel.

Kwanza hakikisha uwanja mpya wa mpira wa kisasa wa Olmotonyi unajengwa mapema kuanzia sasa la sivyo tutashindwa ku-host Afcon in June-Julay 2027.

Pili uhakikishe barabara ya njia sita kutoka Arusha hadi Moshi inakamilika mradi huu ulisimamishwa kuanzia 2015.

Tengeneza metropolitan ya Arusha-Moshi iwe tourist hub ya Afrika. Hii natural confluence iliyopo katikati ya miji hii miwili haipo pengine Afrika na ni potential kubwa ajabu, take that advantage.

Tatu hakikisha kituo kipya cha mikutano cha Kilimanjaro International Convention Centre kinajengwa mapema na kwa ubora wa hali ya juu.

Makonda weka express train Moshi-Arusha, ni takriban 75km kwani watu wengi sana tunataka kuishi Moshi na kufanya kazi Arusha au kinyume. Tunaweza kuiita treni ya Makonda kama itafanikiwa. Unaonaje?

Makonda hakikisha ujenzi wa stendi mpya na ya kisasa Arusha unafanyika vizuri na kukamilika haraka, iwe ya kipekee na sio lazima iwe na maghorofa yasiyotumika kama stendi ya JPM Mbezi.

Watu wanataka kuona Arusha ya kweli ya kimataifa; hakikisha taasisi za Africa Mashariki na zile za Afrika nzima zilizopo Arusha zinapatiwa ardhi ya kutosha, nyumba nzuri na huduma nyingine nzuri kwa ma-experts wanaokuja kuisha na kufanya kazi Arusha.

Kuwa kwako mkuu wa mkoa wa Arusha hakutakuwa na maana yoyote ile kama hutafanya mipango miji katika jiji la Arusha lililokaa hovyo na lenye vichochoro na makazi yasiyo rasmi kila kona. Jiji la Arusha linahitaji master plan mpya. Maeneo kama Unga Limited na Kwa Muorombo ni aibu kubwa kwa hiyo Geneva of Africa, fumua na suka upya haya maeneo kama wewe kweli ni kiongozi mahiri kama unavyojinasibu.

Makonda hakikisha ile miradi ya nyumba za kisasa na satelaite towns za Arusha zilizoanzishwa na Nehemia Mseshu na kuuwawa na Magufuli zinafufuliwa. Makazi ya Arusha bado ni duni kwa watu wa kimataifa na matajiri wa maeneo hayo ambao wangependa kuisha kama Ulaya.

Makonda uongozi wako Arusha utahesabika sio lolote wala chochote kama hutafanya kazi kuhakikisha utalii hapa Arusha unafanywa professionally, kuna vikampuni vingi vya hovyo vinavyoharibu taswira ya utalii Tanzania, hakikisha kunakuwa na uhakiki wa ubora wa wale wote wanaohusika na tour guiding, ma-tour guide wengi ni wahuni, walevi na vilaza wakubwa na mara nyingi huishia kuwa-harrass watalii.

Hakikisha Arusha inakuwa Geneva of Africa ya kweli. Panua ukubwa wa jiji hadi kukaribia KIA au kuunganisha kabisa na Moshi na kutengeneza a larger metropolitan area. Ongeza barabara za hali ya juu za lami na barabara hizi zipite maeneo yenye makazi ya watu wengi kama Usa River nk. Makonda hakikisha Arusha inakuwa na hoteli za hali ya juu za kimataifa, hakikisha kunakuwa na open spaces (parks) kila baada ya nusu kilometa.

Acha majigambo, fanya hayo hapo juu utaonekana kiongozi kwa standard za Arusha. Pia jua kuwa Arusha ni pagumu zaidi ya Dar, unaweza kuaibishwa na ma-chapaa au ma-chalii wadogo tu hapa mjini.
Arusha Moshi nashauri iwe na njia nane. Nne kwenda nne kurudi. Sita hazitoshi.
 
Hz ni ndoto unaota mkuu,vitu km hvyo labda wazungu warudishwe watutawale Tena ndio wanaweza fanya hayo uliyomwambia huyo mchumia tumbo wa CCM makondaa.

Hawa watu CCM hkn afadhali Wala nafuu wt ni wale wale..
Mwakaa utashaanga haujaishaa kashaamishwa kapewa majukumu menginee..
 
Mwenzio anaangalia miradi ya kumpa teni pasenti na wafanyabiashara wa kuwatisha wampe hela, na wa kujipendekeza pia wampe hela, usidanganywe na sanaa za majukwaani ukadhani ndio ukweli
Makonda huyo nyuma yako hapo
 
Mtu kama hajawai fika Arusha anaweza akadhani ni sehemu kubwa na ya kipekee kweli au akadhani sijui Arusha kuna jambo gani jipya kumbe hakuna ni ushamba tuu hakuna lolote😂😂😂😂😂
Naungana na wewe!
Ushamba wa watu wa arusha kujisifu ni tatizo
 
Kwa kuwa wewe umejinasibu kama rais wa Arusha, basi uzingatie yafuatayo la sivyo hutakuwa na maana isipokuwa a political empty barrel.

Kwanza hakikisha uwanja mpya wa mpira wa kisasa wa Olmotonyi unajengwa mapema kuanzia sasa la sivyo tutashindwa ku-host Afcon in June-Julay 2027.

Pili uhakikishe barabara ya njia sita kutoka Arusha hadi Moshi inakamilika mradi huu ulisimamishwa kuanzia 2015.

Tengeneza metropolitan ya Arusha-Moshi iwe tourist hub ya Afrika. Hii natural confluence iliyopo katikati ya miji hii miwili haipo pengine Afrika na ni potential kubwa ajabu, take that advantage.

Tatu hakikisha kituo kipya cha mikutano cha Kilimanjaro International Convention Centre kinajengwa mapema na kwa ubora wa hali ya juu.

Makonda weka express train Moshi-Arusha, ni takriban 75km kwani watu wengi sana tunataka kuishi Moshi na kufanya kazi Arusha au kinyume. Tunaweza kuiita treni ya Makonda kama itafanikiwa. Unaonaje?

Makonda hakikisha ujenzi wa stendi mpya na ya kisasa Arusha unafanyika vizuri na kukamilika haraka, iwe ya kipekee na sio lazima iwe na maghorofa yasiyotumika kama stendi ya JPM Mbezi.

Watu wanataka kuona Arusha ya kweli ya kimataifa; hakikisha taasisi za Africa Mashariki na zile za Afrika nzima zilizopo Arusha zinapatiwa ardhi ya kutosha, nyumba nzuri na huduma nyingine nzuri kwa ma-experts wanaokuja kuisha na kufanya kazi Arusha.

Kuwa kwako mkuu wa mkoa wa Arusha hakutakuwa na maana yoyote ile kama hutafanya mipango miji katika jiji la Arusha lililokaa hovyo na lenye vichochoro na makazi yasiyo rasmi kila kona. Jiji la Arusha linahitaji master plan mpya. Maeneo kama Unga Limited na Kwa Muorombo ni aibu kubwa kwa hiyo Geneva of Africa, fumua na suka upya haya maeneo kama wewe kweli ni kiongozi mahiri kama unavyojinasibu.

Makonda hakikisha ile miradi ya nyumba za kisasa na satelaite towns za Arusha zilizoanzishwa na Nehemia Mseshu na kuuwawa na Magufuli zinafufuliwa. Makazi ya Arusha bado ni duni kwa watu wa kimataifa na matajiri wa maeneo hayo ambao wangependa kuisha kama Ulaya.

Makonda uongozi wako Arusha utahesabika sio lolote wala chochote kama hutafanya kazi kuhakikisha utalii hapa Arusha unafanywa professionally, kuna vikampuni vingi vya hovyo vinavyoharibu taswira ya utalii Tanzania, hakikisha kunakuwa na uhakiki wa ubora wa wale wote wanaohusika na tour guiding, ma-tour guide wengi ni wahuni, walevi na vilaza wakubwa na mara nyingi huishia kuwa-harrass watalii.

Hakikisha Arusha inakuwa Geneva of Africa ya kweli. Panua ukubwa wa jiji hadi kukaribia KIA au kuunganisha kabisa na Moshi na kutengeneza a larger metropolitan area. Ongeza barabara za hali ya juu za lami na barabara hizi zipite maeneo yenye makazi ya watu wengi kama Usa River nk. Makonda hakikisha Arusha inakuwa na hoteli za hali ya juu za kimataifa, hakikisha kunakuwa na open spaces (parks) kila baada ya nusu kilometa.

Acha majigambo, fanya hayo hapo juu utaonekana kiongozi kwa standard za Arusha. Pia jua kuwa Arusha ni pagumu zaidi ya Dar, unaweza kuaibishwa na ma-chapaa au ma-chalii wadogo tu hapa mjini.
Hii ni akili au tope? Katika yote uliyoorodhesha hakuna hata moja linaweza kufanikiwa sababu makonda ni mkuu wa mkoa. Sasa sana anachoweza kufanya ni kuchochea wizi wa kura kwenye chaguzi.
 
Makonda kwanini haachwi kwenye uongozi ikiwa hafai?

Nadhani Makonda anafaa ndio maana anateuliwa angekua hafai mbona watu wa kuteua ni wengi sana kwanini yeye? Maana yake anakitu ambacho wengine hawana.

Aliachwa tangu 2020 lakini Bado imeonekana anahitajika. Tusiompenda sasa tutabaki tu kuhamisha magori kwamba kaisha kisiasa mara kateuliwa kuwa mwenezi katolewa uenezi Kuna wanaofurahi. Kawa mkuu wa mkoa tunaanza utabiri wa atatoka lini ni kujifarji tu.

Kama hafai hawezi kuteuliwa na kama kwa mujibu wa mteuaji anafaa atateuliwa achilia mbali kuumia roho kwa wengine na kuona wivu.

Huenda Makonda akawepo kwenye uongozi kwa muda mrefu na ili usiumie roho ukafa mapema ni kukubali tu kwamba yupo na atakuwepo kadiri inavyompendeza mteuaji.

Huenda mwanzo mteuaji aliambiwa huyo hafai lakini alioambiwa wanafaa wanaharibu zaidi akaona zakuambiwa changanya na zako kamteua.
 
"Kama akifanya" is right.

Akifanya hata robo ya aliyoahidi atakuwa amefanya mengi kuliko marais na mawaziri wengi wa nchi hii na Afrika kwa ujumla.

Sijawahi kusikia kiongozi anaeamini nchi hizi za dunia ya tatu umefika wakati kufuta squatters and slums, kufuta uswahilini. Wataalam wa Mipango miji Makonda anawaambia wanaona uswahilini zinaanzishwa mbele yao, vichochoro na mifereji ya maji machafu ya uswekeni, zinajengwa wanaziangalia, ni wataalam mipango miji wa kubumba. Acha aendelee kuwachanaaa
!
 
Huyu jamaa binafsi nitampa ushirikia na kumuombea kwa Mungu.

Amsamehe mapungufu yake, lakini aendelee kumpa hekima zaidi. Kuna mambo ni sababu ya umri wake. Lakini walau unaona anajua kuweka strategy ya mambo.

Comrade Makonda, you are in my prayers.
 
Huyu jamaa anajua Kula pesa ya umma

Pesa anaanza kupiga hapo katika ziara, atapiga pesa binafsi mno mbali na gharama za msafara
Wakikaa ofisini tunasema watoke ofisini, hela za Halmashauri zinapigwa kwenye ma saiti ya miradi hawana habari, wakifanya ziara tunasema Makonda anapiga hela za ziara.... Afanyeje?

Ziara mkoani zinamfanya azidi kujua nini kinaendelea mitaani na vijijini kwa wananchi. Makonda ameongelea changamoto na vitongoji vya Arusha kwa majina kama mwenyeji. Watumishi Arusha amewaambia wewe na wewe nakujua kwa jina. He is 100% plugged in.

Two three weeks ago Rais alikuwa anaapisha wakuu wa wilaya kwenda Mtwara. Akawa hajui maeneo ya kusini anakomtuma DC mpya akashughulikie magaidi, akasema "sijui wapi kule... " Chairwoman of statehouse national security briefings, hujui wapi Watanzania wanauliwa na magaidi kutoka Capo Delgado! Show respect for your fallen citizens, do your homework, for the love of God. Mwingine akawa anamwapisha kwenda Songea, akamwambia Songea hakuna changamoto! Wapi duniani, no less third world hii, hakuna changamoto ? Hahahahahaaaaaa.... Na kama Songea hakuna changamoto unapeleka DC wa nini? Na RC, na RAS, DED, RPC, OCD, DSO wa nini ???

Acha Paul Makonda awafundishe kufahamu nini kinaendelea mitaani na vijijini, awafundishe kazi. He has his thumb on the pulse of the nation.
 
Siku za nyuma tuliona hapa Dar wakati wa kutiliana saini ujenzi wa uwanja wa Samia Suluhu Hassan utakao jengwa huko Arusha waziri wa michezo alikuwa akilalamika kuwa kuna watendaji walitaka kukwamisha zoezi hilo hadi kutaka kutoleta eneo la tukio viambata vya ardhi.

Ndugu Makonda baada ya kuisha sherehe za Eid tafadhali weka kambi ofisi za ardhi hapo Arusha nadhani utajionea madudu mengi.

Lengo langu nini? hao wahuni wachache wanao endekeza na walio zoea michezo ya kihuni kama hiyo ya kurudisha nyuma maendeleo kwaajili ya matumbo yao tuwaone mahakamani siku moja.

Na Imani nawe Makonda utaunyoosha huo mkoa hata siku ukiondoka umeacha alama ya utendaji uliotukuka.
 
Hii ni akili au tope? Katika yote uliyoorodhesha hakuna hata moja linaweza kufanikiwa sababu makonda ni mkuu wa mkoa. Sasa sana anachoweza kufanya ni kuchochea wizi wa kura kwenye chaguzi.
Sasa anajigamba nini kama hawezi kufanya hata moja ya hayo.
 
Back
Top Bottom