Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Kwenye heading hiyo orodha umechanganya wazalendo na dikteta mmoja na mtuhumiwa mmoja wa mauaji na ujambazi.
 
🚮🚮🚮🚮
 
Mtakuwa mumemuweka kwenye list Kwa sababu za Kisiasa Ili mumuangishe kuelekea 2030.

Huyo Mtani wako ni Moja ya Waandamizi na wapambanaji wa Rais.

Mwisho kwani lazima mtu akubaliane na Kila kitu anachotaka Rais? Kwa Asili ya huyo Mtani wako ni mkatili ila hawezi kutokana na msimamo wa Rais.

Mwisho spana zimekolea maana alichoongea huyo Mtani wako ni kweli tupu.

View: https://twitter.com/mwigulunchemba1/status/1779445799375536509?t=d4BGMWyBuJsH1jNcNL-9ng&s=19
Kazi inaendelea 👇👇

View: https://twitter.com/mwigulunchemba1/status/1779753233998565886?t=iHZheMQU1mlNAftGF2eSnA&s=19
 
Anachapa barua za Katibu, UWT jana nimeona posho zenu zimetoka
 
Baada ya kumjua Mmoja Wao GENTAMYCINE kuanzia sasa nimeamua kutoamini Mtu yoyote kuanzia Ndugu hadi Marafiki.
 
Wakuu,

Hivi mliwahi kushuhudia uenezi wa hao jamaa?

Hao alikua akiwa sehemu akiropoka au kuongea la maana mitandao na vyombo vya habari vyote inakua ndio taarifa muhimu.

Sasa mwenezi kama makala kweli yaani hata vyombo kureport habari zake wanaona uvivu tu.

Hao wenezi Kwa mfano Nape nakumbuka mapinduzi makubwa aliyafanya ikiwapo kuchagiza siasa za vyuo vikuu na siasa za mitandaoni.

Polepole naye alikuja speed sana na alikubalika mno alijichanganya na makundi yote na alikubalika, makonda ndio huyo mliona mikutano yake anakusanya vijiji na vijiji, nadhani ifikie mahala hao watu wasiokubalika wapewe ubalozi au hata uenyekiti wa bodi tu wajipumzikie huko.
 
Chawa Pro Max
 
Hili ni funzo kwa Makonda afuatilie mikutano ya Kinana na Nchimbi atagundua yeye alikuwa ni mwenezi

1: Mropokaji kila jambo anaropoka kwa maslahi yake
2- Mwenezi wa kujikweza na maagizo yasiyo na kichwa wala miguu anamwagiza waziri mkuu; mawaziri; wakuu mikoa ; wilaya ; wakurugenzi na MA RPC
3- Mwenezi asiyeheshimu ofisi za Chama chake yeye anakutana na viongozi barabarani
4- Mwenezi wa Kero za mchongo ili achangishe fedha
5- Mwenezi asiyeheshimu muhimili wa mahakama
6- Mwenezi wa sinema za kupanda ngamia; mkokoteni utoto mwingi

Angalia ziara za kinana na nchimbi hazina hayo yote antamka eti sijajifunza lolote.

Tulia fanya kazi siyo kuropoka huko monduli unachafua hali hewa nchi
 
Wewe mbona umekimbilia humu kuandika maoni hapa huku ukisahau kwamba, kila mtu na namna yake ya anavyoweza kushughulikia jambo

Wewe unanamna yako, nao unaowasigu wanananmna yao, unataka watu wote tuwe kina Makala linapokuja jambo la kudili na kero?

Wasomi wetu mnawehuka baada ya utafiti wenu uchwara?

Ulishawahi ona wapi watu woote tufanane kwenye mitazamo?
 
hao ndugu zako hawana mvuto kwa siasa za hapa, Tanzania imejaa viongozi wezi, wavivu, wazembe n.k wanahitaji mtu wa kariba ya Makonda huko chamani na serikalini...dhambi haichekewi mkuu
 
Bado tu mpo na Makonda!?,hamuoni mnamuongezea mileage!?,tangu jamaa arudi huwezi kuingia JF-siasa ukakosa thread mpya ya Makonda. Great minds discuss ideas, average minds discuss events, WEAK minds discuss PEOPLE.... Eleanor Roosevelt
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…