Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Ili uweze kufanya comparison .kusud ukitoa hukum utoe ya kweli.alete na comparison ya views za YouTube baina ya mwenez aliyepo na aliyepita
Wewe mbwiga kura za CCM haziko YouTube bali ziko kwa wananchi
 
MAkonda baba lao
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
hao ndugu zako hawana mvuto kwa siasa za hapa, Tanzania imejaa viongozi wezi, wavivu, wazembe n.k wanahitaji mtu wa kariba ya Makonda huko chamani na serikalini...dhambi haichekewi mkuu
Mliwahi kumuuliza juu ya nyumba aliyosema ilibidi asitumie mahakama ili kuimiliki aliijenga lini? Mtu asiyetaka haki ipatikane kupitia vyombo vya kisheria, utamtoa kwenye kundi la wote uliowataja hapo?
 
We huijui arusha na Kuna uwezekano unaishiaga stendi tu watalii wanakaa Arusha hata wiki tatu wakiwa mjini tu we unasema Arusha mjini hakuna utalii kwanza Hali ya hewa tu ya Arusha ni utalii tosha ni perfect weather, Kuna themi falls, cultural heritage, via via, Mt suye, themi living garden unajua Arusha pale Kuna sehemu city center unaweza kuingia ukadhani uko amazon forest na sasa hivi wanaiboresha kutengeneza sehemu za mapumziko kinachokosekana Arusha ni miundombinu tu otherwise Arusha Ina Kila sifa ya kuwa world-class destination na serikali sijui hawalioni hili sehemu inayoingiza pesa nyingi kuinvest ili wapate hela nyingi zaidi jiulize kakonko Kuna stendi Kali lakini hata haitumiki bado watu wanaenda stendi ya zamani wamepoteza hela nyingi sehemu kusiko na mahitaji lakini Arusha kwenye mahitaji hakuna stendi Wala masoko mapya bila kufahamu aibu ya Arusha ni aibu ya watanzania wote hiyo asilimia 80% ya watalii wanaoenda mbugani kupitia Arusha wakifika kwao hawasemi Arusha ya hovyo watasema Tanzania ya hovyo
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda akieleza mkakati wa kupambana na dawa za kulevya Arusha akirejea namna alivyopambana na uhalifu huo wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkakati huo ameutoa wakati akizungumza na uongozi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha ukiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa ACP Justine Masejo, Wakuu wa Polisi na wapelelezi kutoka wilaya zote za mkoa huo Jumamosi Aprili 20, 2024.

Your browser is not able to display this video.
 
Paul Makonda ndiye Mkuu wa Mkoa mbumbumbu zaidi hapa Tanzania kwa sasa.
Yaani kwa yote hayo aliyopitia huko siku za nyuma bado tu hajajifunza kitu?????
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa!
 
Samaki anayefungua mdomo hunaswa na ndoano..
 
Ifike wakati sasa Makonda anyamaze au anyamazishwe , hawezi kuendelea kudanganya umma halafu tukamkalia Kimya , Uongo wake ufike mwisho , na aache kutafuta huruma .

Ameendelea kusema Uongo huko Arusha kwamba aligombana na Wauza madawa ya kulevya na kwamba amenusurika kuuawa mara kadhaa , sasa alinusurika wakati ule wa Magufuli au ni lini ? Mbona akiwa Mwenezi nako alisema amenusurika kuuawa , sasa tushike lipi ? Binafsi napinga madai yake na Simuaamini hata Chembe .

Wauza madawa aliowasingizia hawa akina Wema Sepetu , Nyandu Tozi na TID ndio waliotaka kumuua ? au ni akina Manji ambao waliwekwa ndani kwa muda Mrefu au ni wepi wengine ?

Ukweli ni huu hapa , Katika madaraka yake madogo aliyopewa Makonda aligombana na kila Mtu , Alipogombana na Chongolo kule Kinondoni anataka kusema naye alikuwa muuza Unga ? Alipogombona na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea hadi kupelekana Mahakamani ilikuwa sababu ya Unga ? Alipompiga Ngwala Mzee Warioba anataka kusema naye alikuwa Muuza Unga ? Alipovamia Clouds media huko nako walikuwa nauza unga ? Tukiandika watu aliogombana nao Makonda humu JF Itajaa na wala haitatosha , Makonda alipiga Marufuku Wabunge kuishi kwenye Mkoa aliokuwa RC , na kwamba wanatakiwa kuwa Dodoma ile amri nayo ilihusu Wauza unga , Mbunge Aeshi alilalamika Bungeni kwamba aliambiwa na Makonda akigusa Dar atashughulikiwa , huyu naye alikuwa Muuza Unga ? Alipodhulumu nyumba ya GSM Block 41 Kinondoni atuambie kama huyu naye alikuwa Muuza Unga ?

Je hakukuwa na Wakuu wa Wilaya au Wakuu wa Mikoa wengine ilikuwaje yeye Makonda ndio agombane na kila mtu , ilikuwaje yeye awe anadhalilisha kila mtu bila Ushahidi wowote ?

Leo analialia ili aonewe huruma na nani ili iweje , Yeye ni kiongozi wa CCM mtoto mpendwa wa Mama kama anavyojinadi yeye mwenyewe , Kwanini asimuambie Mama yake ambaye ndio Amiri Jeshi Mkuu ili awakamate na kuwashughulikia hao wanaotaka Kumuua mara zote hizo ?

Makonda usitupotezee muda kama umeshindwa Uongozi Jiuzulu urudi mitaani .

 
Bwana we,Makonda kama kweli unahitaji Kupambana naye Kwa maneno lazima uwe naye Ground Zero na uende naye Bampa tu Bampa.Kupambana na Makonda nyuma ya Keyboard hakuna anayemuweze kwa Tabia zenu za Kinafiki na uoga.

In short Bada hakuna anayeweza kudeal na Makonda na Akamnyamazisha.Hata Magufuli Mwenyewe Alishindwa Sembuse WEWE.

Tafuta Kazi ingine Ufanye au kama unataka Kudeal Naye WEWE ita Press Nenda Nae Level tena Kwa kumuanza Kabisa na SIO kusubiri Mpaka aonge umjibu kama vile wewe kazi yako ni kuimba Kiitikio na yeye kuweka Mashairi.

Tulia DAWA iingiae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…