Ifike wakati sasa Makonda anyamaze au anyamazishwe , hawezi kuendelea kudanganya umma halafu tukamkalia Kimya , Uongo wake ufike mwisho , na aache kutafuta huruma .
Ameendelea kusema Uongo huko Arusha kwamba aligombana na Wauza madawa ya kulevya na kwamba amenusurika kuuawa mara kadhaa , sasa alinusurika wakati ule wa Magufuli au ni lini ? Mbona akiwa Mwenezi nako alisema amenusurika kuuawa , sasa tushike lipi ? Binafsi napinga madai yake na Simuaamini hata Chembe .
Wauza madawa aliowasingizia hawa akina Wema Sepetu , Nyandu Tozi na TID ndio waliotaka kumuua ? au ni akina Manji ambao waliwekwa ndani kwa muda Mrefu au ni wepi wengine ?
Ukweli ni huu hapa , Katika madaraka yake madogo aliyopewa Makonda aligombana na kila Mtu , Alipogombana na Chongolo kule Kinondoni anataka kusema naye alikuwa muuza Unga ? Alipogombona na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea hadi kupelekana Mahakamani ilikuwa sababu ya Unga ? Alipompiga Ngwala Mzee Warioba anataka kusema naye alikuwa Muuza Unga ? Alipovamia Clouds media huko nako walikuwa nauza unga ? Tukiandika watu aliogombana nao Makonda humu JF Itajaa na wala haitatosha , Makonda alipiga Marufuku Wabunge kuishi kwenye Mkoa aliokuwa RC , na kwamba wanatakiwa kuwa Dodoma ile amri nayo ilihusu Wauza unga , Mbunge Aeshi alilalamika Bungeni kwamba aliambiwa na Makonda akigusa Dar atashughulikiwa , huyu naye alikuwa Muuza Unga ? Alipodhulumu nyumba ya GSM Block 41 Kinondoni atuambie kama huyu naye alikuwa Muuza Unga ?
Je hakukuwa na Wakuu wa Wilaya au Wakuu wa Mikoa wengine ilikuwaje yeye Makonda ndio agombane na kila mtu , ilikuwaje yeye awe anadhalilisha kila mtu bila Ushahidi wowote ?
Leo analialia ili aonewe huruma na nani ili iweje , Yeye ni kiongozi wa CCM mtoto mpendwa wa Mama kama anavyojinadi yeye mwenyewe , Kwanini asimuambie Mama yake ambaye ndio Amiri Jeshi Mkuu ili awakamate na kuwashughulikia hao wanaotaka Kumuua mara zote hizo ?
Makonda usitupotezee muda kama umeshindwa Uongozi Jiuzulu urudi mitaani .
View attachment 2969272