Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda ndiye Mkuu wa Mkoa mbumbumbu zaidi hapa Tanzania kwa sasa.
Kuna msemo wa Kiswahili unaosema kwamba "Debe tupu haliachi kuvuma."
Kabisaa yaani debe tupu linawaumiza watu na ma vyeo yao kazi kuimba taarabu kulihusu debe tupu ...MAKONDA BOMAYEEE hata wakupe ubalozi wa mtaa bado utawatikisa tu,,,,tatizo nyota
 
Big up Makonda! God bless you.
 
Wenye chuki binafsi na Mheshimiwa Makonda watakufa kwa presha mwaka huu.
Nyinyi Chawa wa Paul Makonda mnajisumbua Sana, ukweli ni kwamba mtu huyu amejitengenezea maadui wengi sana hapa Tanzania na duniani kote kwa ujumla, amejichafua na amechafuka vibaya sana kutokana na sababu hiyo. Hadi sasa, hakuna "sabuni" yoyote ile ambayo ina Uwezo wa kumsafisha au kumtakasa huyu mtu. Mnajisumbua bure kabisa kumpigia debe mtu huyu.
Hata ndani ya CCM yenyewe ana maadui wengi sana, na watu wengi hawamtaki, isipokuwa wameamua kukaa kimya kwa sababu Mwenyekiti wao wa Chama ndiye aliyemteua huyu mtu.
 
Amejichafuaje? Kutetea wanyonge ndio kujichafua? Kutaka watumishi wa umma wawajibike na kutekeleza majukumu yao ndio kujichafua? Kutaka haki itendeke na wanyonge kutendewa haki ndiko kujichafua?
 
Ngada na ufipa tena,ni kama maji na samaki
 
Tulijua Chawa wake watakuja na tuko tayari kupambana nao kwa hoja au kivyovyote
Huna hoja kibwengo wewe,mmeandika sana kuhusu dogo lakini mmechemka,mmeishia kujitekenya na kucheka wenyewe tu,jamaa habadililiki na kasi yake ndio kwanza inaongezeka maradufu
 
Amewataha mawaziri wanaofadhili mama yake kutukanwa?
Maana ishara ya mwongo mwongo ni kuahirisha ahadi ili zama zibadilike.
Jumatatu alioahidi bado?
 

Nakuona mama kigani wa kambo unamtega Bebe wako😀😀😀
 
Na yule Daudi Albert Bashite, kijana aliyetokea Kijiji cha Kolomije kule Shinyanga/Simiyu, ni jana, leo na juzi, au?
 
Mleta mada huyo DAB ni bado kijana??
Au huko CCM kila mtu ni kijana maana hata Makala naye mnamwita kijana.
Nchimbi naye unamwita kijana
Toeni tafsiri ya neno kijana kwa nyie watu wa Lumumba??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…