Ndugu zangu Watanzania,
Leo kule kanda ya kaskazini mkoani Arusha Mwamba Mwenyewe Makonda kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara aliwakutanisha watumishi na watendaji wote wa mkoa wa Arusha katika kikao maalum cha kutoa Dira na taswira ya namna ambavyo angetaka mkoa wa Arusha uwe,pamoja na kumtaka kila mtumishi na mtendaji wa serikali kutekeleza wajibu wake kikamilifu.
Amesema yeye ni yule wa jana,leo na hata milele na kwamba hakuna copy ya Makonda kwa maana kwamba makonda uliyemuona jana ndio yule wa leo na wa kesho na hata akiondoka atabakia kuwa na kusomeka hivyo. Amewataka watumishi wa umma kuchapa kazi kwelikweli bila kulega lega wala kutengenezeana ajali za kazini.amesema ni lazima kushirikiana kwa pamoja na siyo kuchongeana au kukwamishana.
Amesema ya kuwa yeye hana muda wa kumvumilia mtu kazini bali anataka mtu aliye kamilika na tayari kwa kazi.amesema yeye hanaga habari za kusema ngoja tumvumilie mtu kwa matarajio kuwa atabadilika baadaye .amesema yeye hana huo muda na wala hajajaliwa kipawa hicho.amesema kuwa yeye mwenyewe utendaji wake unapimwa kwa siku.amewaomba msamaha mapema kabisa watumishi na watendaji wazembe kuwa hatawavumilia hata kidogo na badala yake wabadilike haraka sana.
Amesema kuwa ni lazima kila mtu ahakikishe kuwa anaenea vyema katika nafasi yake na yule ambaye haenei vizuri atafute vitu vya kumsaidia kuenea ,na asipofanya hivyo atamlazimisha aenee vizuri.amesema amechelewa sana na hivyo hayupo tayari kuona akikwamishwa na mtu yeyote yule.
Mwamba Makonda amezungumza mengi sana tena sana katika siku ya leo katika kutoa Dira na muelekeo wake ikiwa ni pamoja na kuhimiza umoja na mshikamano katika kufanya kazi ,na siyo kufanya kazi utafikiri unakimbiza mwenge.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.