Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Wakati Benjamin William Mkapa akiwa Mhariri wa Magazeti ya Serikali, akiwa katika kazi yake, alisikia maneno ya waziri mmoja, Oscar Kambona, akimsengenya rais, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Benjamin Mkapa hakupanda kwenye jukwaa lolote la kisiasa na kutoa habari hizo. Alimfuata rais Nyerere na kumpa hizo habari. Nyerere akamuhoji akitaka kujua uhakika wa habari hizo, kwa sababu aliona itakuwa vigumu sana kwa Kambona kumsema yeye Nyerere vibaya, akizingatia urafiki wao wa muda mrefu.

Kama mwanafalsafa aliyefuata methali ya Kirusi "Trust but verify", Nyerere alimuamini Kambona, lakini akataka kuhakiki mambo na kuweka watu waliomfuatilia, ambao walikuja kuthibitisha maneno aliyoyasema Mkapa kwa Nyerere.

Kilichofuata ni historia. Kambona alikimbia nchi na kwenda uhamishoni Uingereza alikokaa kwa miaka mingi sana.

Historia hii inatufundisha nini?

Kukosana viongozi kushawahi kutokea nchi hii, ila hakukutangazwa kwenye hotuba. Kutangaza kwenye hotuba ilikuwa ni papara inayoonesha kukosa mahesabu kama aliyokuwa nayo Benjamin William Mkapa.

Hii ndiyo tofauti ya mtu kama Mkapa aliyepanda ngazi mpaka kuwa rais na mtu kama Makonda ambaye anatafuta kiki za muda bila ya kuusoma mchezo wa muda mrefu.
Hatari kweli kweli.....ila Kambona amezushiwa mengi sana na kiini cha mgogoro wake na Mwl imebakia fumbo lisilo na jibu, ila jaribio la mapinduzi liliofeli mwaka 1964 limeficha mengi.

JokaKuu Mag3 zitto junior Pascal Mayalla Nguruvi3
 
Huwa mna mtabiri sana lakini huyu mtu si kwamba kathibitsha tu hatabiriki,ila inaonekana kabisa ana kitu cha tofauti na vijana wengi wanachokiona wanaomteua tu.

Nasisitiza vijana wenzangu,kuwa wakweli hadharani na sirini,kuwezi waaminifu kwa walio waamini,na hakikisheni mnakuwa na utu kama kuchukua hatua mumeshindwa.
 
Makonda ana narcissistic traits, hata kama anapenda maendeleo kuna kale ka kujiona flani hivi, ndo maana ziliiva na jiwe.
 
Huwa mna mtabiri sana lakini huyu mtu si kwamba kathibitsha tu hatabiriki,ila inaonekana kabisa ana kitu cha tofauti na vijana wengi wanachokiona wanaomteua tu.

Nasisitiza vijana wenzangu,kuwa wakweli hadharani na sirini,kuwezi waaminifu kwa walio waamini,na hakikisheni mnakuwa na utu kama kuchukua hatua mumeshindwa.
Makonda ukikutana naye Uso kwa uso na mkaongea ni Mtu mmoja mpole mnyenyekevu na anajali sana..
Tofauti na Makonda unayemuona Kwenye Mitandao na Kwenye Majukwaa
 
Paul makonda lazima alikwea kizimba. Wengi hatujui nini kinahojiwaga na muhojiwa anapaswa kutwii vipi. Ila kwa Paul lazima atakuwa na kujiona ni mteule.

Kiufupi ajitathimini sio kila nyakati unapaswa kufanya kila kitu.

Nahisi saa 3 za mahojiano alipata kibano kwa maneno na kuona anaweza akafanya apendavyo.

Binafsi sion kama anafanya sawa au sisawa ila ana hulka ambayo sidhani kama ataicha... tabia zingine ni za kuzaliwa nazo. Huwez tegemea mtu akaiacha kirahisi.

Kimsingi tume ilipaswa kumuita tangu alivyoanza kuwapigia simu mawaziri.....

Moja wa mawaziri aliowapigia simu hadharani akitoa oda ni Mama wa afya bi Ummy...Huyu wa ardhi jamaa wa ukonga. Na baadhi wachache aliowamudu. Hakuweza kumpigia mH waziri mkuu na makamu mzee mpango. Ila nahisi alitamani apande juu juu zaidi yao.wote isipokuwa Mama pekee.

Kwa hiyo siamini kuwa atakuja badilika japo masaa aliyowekwa si kitu chepesi. Alitoka jasho
Ccm acheni kutufanya Watz wajinga.
 
Hili swali najiuliza sana na hasa ninaposikia Makonda ataongea na Waandishi wa Habari siku za karibuni

Bado sijaelewa Wananchi watapenda kufuatilia Habari gani Kati ya Maandamano ya Tundu Antipas Lisu na Sarakasi Sanaa za Lumumba

Ngoja tuone 🐼
 
Hatari kweli kweli.....ila Kambona amezushiwa mengi sana na kiini cha mgogoro wake na Mwl imebakia fumbo lisilo na jibu, ila jaribio la mapinduzi liliofeli mwaka 1964 limeficha mengi.

JokaKuu Mag3 zitto junior Pascal Mayalla Nguruvi3
Mkuu Proved , ni kweli Kambona amesingiziwa mengi!. Mkuu Kiranga, unapoleta habari za tuhuma nzito kama hizi za u snitch, pia taja source na proof, kitendo cha kumtuhumu mtu ambaye ni marehemu kuwa ni snitch, bila ushahidi wowote, wakati hawezi kujitetea, sio kumtendea haki!.
P
 
Kwani kuna shida gani? Hivi wewe jamaa mbona una cheap politics namna hii. Wala hakuna anayewaza hayo uyawazayo. Chadema wana ratiba yao na mipango yao wala havihusiani na hicho kikao cha ndani cha CCM.
Hili swali najiuliza sana na hasa ninaposikia Makonda ataongea na Waandishi wa Habari siku za karibuni

Bado sijaelewa Wananchi watapenda kufuatilia Habari gani Kati ya Maandamano ya Tundu Antipas Lisu na Sarakasi Sanaa za Lumumba

Ngoja tuone 🐼
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewasili kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili.

Makonda ameitikia wito wa kufika mbele ya kamati hiyo kwa barua aliyoandikiwa Aprili 16, 2024 huku sababu za kuitwa kwake zikiwa hazijawekwa wazi.

Awali, Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 kabla ya kusogezwa mbele na kupangwa kufanyika leo Jumatatu, Aprili 22, 2024.

Pia soma
Angewataja vipi na Hana ushahidi…
 
Mkuu Proved , ni kweli Kambona amesingiziwa mengi!. Mkuu Kiranga, unapoleta habari za tuhuma nzito kama hizi za u snitch, pia taja source na proof, kitendo cha kumtuhumu mtu ambaye ni marehemu kuwa ni snitch, bila ushahidi wowote, wakati hawezi kujitetea, sio kumtendea haki!.
P
Mkuu,

Source nilishaweka kitabu mpaka kurasa post #18.

Kitabu kilichapishwa mwaka 1971 -722 kinaitwa "We Must Run While They Walk: A Portrait of Africa's Julius Nyerere" by William Edgett Smith 1971 alternatively published as "Nyerere of Tanzania" in the UK in 1972.

Pia, mtu ambaye kazi yake ilikuwa kukusanya na kuhariri habari kumuita snitch kwa kufanya kazi yake wewe ndiye unamvunjia heshima.

Post in thread 'Mzee Hashim Rungwe: Makonda anataka awe chawa mkuu wa Rais Samia, analazimisha asikilizwe yeye sana' Mzee Hashim Rungwe: Makonda anataka awe chawa mkuu wa Rais Samia, analazimisha asikilizwe yeye sana
 
Back
Top Bottom