Makonda kaitwa, kaitikia!
Tarehe 12 April Makonda alisikika na kuutangazia umma, mbele ya Rais Sami, alisema:
" Nawajua kwa majina na leo tarehe 12 April, nataka iwe mwisho kuwatukana watu kwenye mitandao ya kijamii kumtukana Rais Samia na jumatatu ,tarehe 15, ikiendelea, nataja majina, wengine ni mawaziri"
Bomu likatulia
Kamati ya maadili ya CCM, chini ya mzee Kinana ikaamua kukata mzizi wa fitna.
Makonda akaitwa Dodoma, mnele ya Kamati ya Maadili.
Kaanza mzee Kinana, ehee mwakwetu Makonda, tutajie wale mawaziri wanaomchafua Mama Samia kwa kuwatumia watu mitandaoni.
Makonda: unajua....eeeh, wafahamu.....eeeh, ninyi ndio mna vyombo vyote. Chunguzeni.
Mzee Kinana: si ulisema utawataja?
Wataje sasa ili tuwaangushie jumba bovu!
Makonda: .....unajua mzee, mambo haya...., lakini......!
Kinana : Kama ulitoa kauli zile kujikomba hebu sema tu!
Habari ni kwamba Makonda kahojiwa masaa matatu, na kwa kibaridi cha Dodoma, alikuwa anasweti muda wote.
NB : fuatilia gazeti Mwananchi leo 23 April,
Angalizo: chumvi ni zangu mwenyewe.