Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

On a serious note Hawa kina rungwe ndo machawa wakuu wa ccm, nani hajui kua hivyo vyama vyote vishakua ccm b, ikifika chaguzi wanapewa hela na ccm ili nchi ionekane Ina demokrasia kwa kusimamisha vyama 16 vya upinzani kwenye uchaguzi
Badala ya kupambana na CCM wanazungumzia mada zisizo na maana kwa upinzani.
 
Huyu Mzee hua ananiacha hoi sana, Kuna siku alihojiwa akaulizwa unazungumziaje hali ya sasa ya maisha ya watanzania.... Akajibu


"Mimi niliwaambia wanichague Mimi wawe wanakula ubwabwa bure na matunda Kila Kona niliwaambia ntawapandia miti wakakataa, waache wapambane"
Alisema wacha wale tozo
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewasili kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili.

Makonda ameitikia wito wa kufika mbele ya kamati hiyo kwa barua aliyoandikiwa Aprili 16, 2024 huku sababu za kuitwa kwake zikiwa hazijawekwa wazi.

Awali, Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 kabla ya kusogezwa mbele na kupangwa kufanyika leo Jumatatu, Aprili 22, 2024.

Pia soma
Ukiachana na ujana,Makonda ni jembe na anaweza kuongoza nchi
 
Sema uongo uko wapi, halafu onesha ukweli.

Unachobisha nini sasa? Hujui kuwa wakati huo miaka ya 1960 wakati Kambona anagombana na Nyerere Mkapa alikuwa Mhariri wa magazeti ya serikali?

Unachosema uongo ni kipi? Kwamba Mkapa hakuwapo serikalini wakati Kambona anagombana na Nyerere?

Kasome kitabu kinaitwa "Nyerere of Tanzania" cha William Edgett Smith, kuanzia ukurasa wa 189 uone habari nzima ilivyotokea na Mkapa alivyoifuatilia na kumuhakikishia Nyerere.

Unayoyaongea yana ka ukweli fulani, Inafahamika wazi kuwa MKpa alikuwa ni Chawa wa Nyerere
 
Makonda kaitwa, kaitikia!

Tarehe 12 April Makonda alisikika na kuutangazia umma, mbele ya Rais Sami, alisema:
" Nawajua kwa majina na leo tarehe 12 April, nataka iwe mwisho kuwatukana watu kwenye mitandao ya kijamii kumtukana Rais Samia na jumatatu ,tarehe 15, ikiendelea, nataja majina, wengine ni mawaziri"

Bomu likatulia

Kamati ya maadili ya CCM, chini ya mzee Kinana ikaamua kukata mzizi wa fitna.
Makonda akaitwa Dodoma, mnele ya Kamati ya Maadili.

Kaanza mzee Kinana, ehee mwakwetu Makonda, tutajie wale mawaziri wanaomchafua Mama Samia kwa kuwatumia watu mitandaoni.

Makonda: unajua....eeeh, wafahamu.....eeeh, ninyi ndio mna vyombo vyote. Chunguzeni.

Mzee Kinana: si ulisema utawataja?
Wataje sasa ili tuwaangushie jumba bovu!

Makonda: .....unajua mzee, mambo haya...., lakini......!
Kinana : Kama ulitoa kauli zile kujikomba hebu sema tu!

Habari ni kwamba Makonda kahojiwa masaa matatu, na kwa kibaridi cha Dodoma, alikuwa anasweti muda wote.

NB : fuatilia gazeti Mwananchi leo 23 April,
Angalizo: chumvi ni zangu mwenyewe.
 
Duh! Aliyeitwa ni Christian Makonda lakini aliyekwenda ni Albert Bashite
 
Nimekuelewa sana chief!

Chumvi ache ziendelee kuwa zako, ngoja tusubiri mbivu na mbichi
 
Makonda jana tulikuwa naye Leaders kumuaga Captain, hayo mahojiano alifanyiwa kwa zoom?
 
Hata kama ningekuwa Mimi nisingekubali kuwataja.maana unaowatajia hawana uadilifu wowote zaidi ya ufisadi tu na uchawa Kwa mwenyekiti wao.mfano kinanana huyu anajulukana tz nzima na kimataifa kuwa ni fisadi namba moja
 
Back
Top Bottom