Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Wakati Benjamin William Mkapa akiwa Mhariri wa Magazeti ya Serikali, akiwa katika kazi yake, alisikia maneno ya waziri mmoja, Oscar Kambona, akimsengenya rais, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Benjamin Mkapa hakupanda kwenye jukwaa lolote la kisiasa na kutoa habari hizo. Alimfuata rais Nyerere na kumpa hizo habari. Nyerere akamuhoji akitaka kujua uhakika wa habari hizo, kwa sababu aliona itakuwa vigunu sana kwa Kambona kumsema yeye Nyerere vibaya, akizingatia urafiki wao wa muda mrefu.

Kama mwanafalsafa aliyefuata methali ya Kirusi "Trust but verify", Nyerere alimuamini Kambona, lakini akataka kuhakiki mambo na kuweka watu waliomfuatilia, ambao walikuja kuthibitisha maneno aliyoyasema Mkapa kwa Nyerere.

Kilichofuata ni historia. Kambona alikimbia nchi na kwenda uhamishoni Uingereza alikokaa kwa miaka mingi sana.

Historia hii inatufundisha nini?

Kukosana viongozi kushawahi kutokea nchi hii, ika hakujutangazwa kwenye hotuba. Kutangaza kwwnye hotuba ilikuwa ni papara inayoonesha kukosa mahesabu kama aliyokuwa nayo Benjamin William Mkapa.

Hii ndiyo tofauti ya mtu kama Mkapa aliyepanda ngazi mpaka kuwa rais na mtu kama Makonda ambaye anatafuta kiki za muda bila ya kuusoma mchezo wa muda mrefu.
Acha uongo kawadanganye walugaluga wenzako huko

Kambona na Mkapa wapi nawapi?
 
Najaribu kuwaza...🤔

Tumeona Makonda akitoa kauli mbalimbali ambazo kimsingi si rafiki Kwa baadhi viongozi wa Chama na zinatishia uwepo wa viongozi hao ndani CCM.

Nina imani Kuna kitu nyuma ya hizi vurugu za Makonda kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 mpaka sasa Kwa kiasi kikubwa jamaa anawatu na kaaminika katika jamii kama mtetezi na msemaji wa watu.

Sasa basi what if?

Kabla ya 2025 Makonda akawajibishwa na Chama kwa kigezo cha "Maadili" na akaamua kujiunga na upinzani mathalani ACT na kugombea Urais, nini kitatokea?

Je, kabla ya kujiunga na ACT akiwa bado yuko huru na akaendeleza harakati zake kama mtu huru je, CHADEMA itakua tayari kumpokea?

Mwisho, what if anatengenezwa kwa ajili ya hayo hapo kuelekea 2025 apatikane mtu wa kichachafya CCM kidogo mwaka 2025 na baadae Mama aseme "We ni mwanangu rudi nyumbani."

Jumatatu njema.
Jinga km Makonda chama gani kitampokea, kwa lipi. We huijui CCM. Lile bwege limeshajichimbia kaburi
 
Hao wanaomuhoji wote wanamuogopa. Itakuwa kama vile wao ndio wanahojiwa.

Makonda ni zimwi la kufugwa ambalo limekuwa kubwa kuliko wanaomfuga.
We ni zombie, nchi hii mkuu wa majeshi ameondolewa, IGP ameondolewa, mkuu wa TISS, katibu mkuu kiongozi aliondoķa km jambazi, Makonda ni takataka gani.
 
Acha uongo kawadanganye walugaluga wenzako huko

Kambona na Mkapa wapi nawapi?
Sema uongo uko wapi, halafu onesha ukweli.

Unachobisha nini sasa? Hujui kuwa wakati huo miaka ya 1960 wakati Kambona anagombana na Nyerere Mkapa alikuwa Mhariri wa magazeti ya serikali?

Unachosema uongo ni kipi? Kwamba Mkapa hakuwapo serikalini wakati Kambona anagombana na Nyerere?

Kasome kitabu kinaitwa "Nyerere of Tanzania" cha William Edgett Smith, kuanzia ukurasa wa 267 uone habari nzima ilivyotokea na Mkapa alivyoifuatilia na kumuhakikishia Nyerere.
 
Makonda anataka yeye ndiye awe chawa mkuu wa Rais Samia, anamlazimisha Rais amsikilize yeye sana kwamba yeye ndiye msema kweli, Mimi kwenye serikali yangu sitahitaji machawa wala watu wakujipendekeza kwangu” Hashim Rungwe

Ninachompendea huyu Mzee achilia mbali tu kupenda jinsi alivyo Mwerevu, mwenye Exposure lakini pia ni Tajiri na Msela.
 
Wakati Benjamin William Mkapa akiwa Mhariri wa Magazeti ya Serikali, akiwa katika kazi yake, alisikia maneno ya waziri mmoja, Oscar Kambona, akimsengenya rais, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Benjamin Mkapa hakupanda kwenye jukwaa lolote la kisiasa na kutoa habari hizo. Alimfuata rais Nyerere na kumpa hizo habari. Nyerere akamuhoji akitaka kujua uhakika wa habari hizo, kwa sababu aliona itakuwa vigumu sana kwa Kambona kumsema yeye Nyerere vibaya, akizingatia urafiki wao wa muda mrefu.

Kama mwanafalsafa aliyefuata methali ya Kirusi "Trust but verify", Nyerere alimuamini Kambona, lakini akataka kuhakiki mambo na kuweka watu waliomfuatilia, ambao walikuja kuthibitisha maneno aliyoyasema Mkapa kwa Nyerere.

Kilichofuata ni historia. Kambona alikimbia nchi na kwenda uhamishoni Uingereza alikokaa kwa miaka mingi sana.

Historia hii inatufundisha nini?

Kukosana viongozi kushawahi kutokea nchi hii, ila hakukutangazwa kwenye hotuba. Kutangaza kwenye hotuba ilikuwa ni papara inayoonesha kukosa mahesabu kama aliyokuwa nayo Benjamin William Mkapa.

Hii ndiyo tofauti ya mtu kama Mkapa aliyepanda ngazi mpaka kuwa rais na mtu kama Makonda ambaye anatafuta kiki za muda bila ya kuusoma mchezo wa muda mrefu.
Wenye uwezo na walisome andiko hili
 
📝🆒👌👆👍👏🤝👊🙏🎁🗼
 
Makonda anataka yeye ndiye awe chawa mkuu wa Rais Samia, anamlazimisha Rais amsikilize yeye sana kwamba yeye ndiye msema kweli, Mimi kwenye serikali yangu sitahitaji machawa wala watu wakujipendekeza kwangu” Hashim Rungwe

MAKONDA MCHONGANISHI SANA ANEUMIZA WATU WENGI KIPINDI CHA UTAWALA KATILI WA MAGUFULI HAFAI KUWA KIONGOZI
 
Back
Top Bottom