Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Tumtafute Mungu wakati anapatikana, na tumwite wakati yuko Tayari....Nimekuwa najiuliza wakati Bashite yupo nje ya Uongozi alikuwa haonekani kuwatembelea viongozi wa dini na kuwataka wamwombee na kumbariki. Mara baada ya Kuteuliwa kuwa Katibu wa Uenezi wa CCM amekwisha watembelea Wafuatao;
1. Kardinal Mstaafu Pengo
2. Sheikh Mkuu Zuberi
3. Askofu mkuu wa Anglican na baada ya kuteuliwa tena kuwa Mkuu wa Mkoa amefanya hivyo hivyo.
Najiuliza ametenda dhambi gani inayomtesa na kumfanya ahangaike hivi kutaka kuombewa? Mbona alipokuwa nje ya uongozi hatukumwona kuwatafuta hawa viongozi wa dini?
Ushauri kwa Bashite: Kama anautafuta wokovu basi awaombe Msamaha kwanza wale wote aliowatendea mabaya katika maisha yake na wakili kuwa wamsamehe ndio aende kwa hao viongozi wa dini bila kufanya hivyo sala na Mikono ya hao Viongozi wa Dini Wanayomwekea kichwani ni kazi bure.
Daima tusichoke kumtafuta Mungu
