Sifa kubwa ya mwanasiasa ni kuwa na uwezo wa kutunga na kubuni sera nzuri bila kusahau kuwa na ushawishi au umaarufu kwa watu, sera nzuri peke yake haitoshi.
Si mtazami makonda kama mwanasiasa bali namtazama kama mwanasaikolojia wa siasa na kijana anayetafuta ridhiki ili ajikimu kimaisha, Licha ya kutokea ktk familia masikini na skendo alizopitia huyu mwamba ila bado anapambana na hakauki midomoni mwa watu kwa kuja na style ndogo ndogo ambazo wengi huziona za kijinga ila ndizo zinazompa umaarufu na kumfanya apate trend
Mwaka 2015 wakati Raisi Magufuli kachukua nchi alitamka kuwa ktk orodha yake ya wakuu wa mikoa itakayotoka mtu pekee ambaye tayari ananafasi kwenye mkeka ni Paul Makonda.
Huyu ndiye mwamba pekee anaeweza kumuweka raisi yeyote close akawa kama mshikaji wake licha ya kuwa na cheo kidogo. Wengi mtachukulia poa lakini ni kazi ngumu sana.
Huyu ndiye mtu pekee Tanzania mwenye uwezo wa kiutrend mwaka mzima.
Yeye siku zote huanzisha trend na ni mjanja mjanja sana anawazidi wanasiasa wengi sana hapo CCM
Mnaikumbuka kauli yake ya juzi kwa raisi samia kuhusu mawaziri wanaolipa watu wamchafue taisi mtandaoni kuwa anawajua na ayawatataja na kuwaonya waache! Ile ni mbinu ya kivita ya kumuweka close mama, wazungu wanasema The enemy of your enemy is your friend
wanasiasa wasaka fursa mnachakujifunza kwa Makonda yule ni mwanasaikolojia wa siasa hawezi kulala njaa mjini.