Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Hakika hiki ni kichekesho! Katika siku muhimu kama Mei Mosi kwa wafanyakazi.wanaowazia hatima ya kazi zao, mishahara na mafao yao ya kustaafu, pension zao, kupandishwa vyeo na kila linalowasibu eti ndio haya tena ya Makonda?
Mbele ya makamu wa Rais anayemwakilisha Rais mnasema bila aibu kuwa Makonda ni mbunifu kisa WADUDU?
Yaani bila aibu mnaleta vijana wakuwapeleka Rehab mbele ya Rais, mabalozi na wakuu wengine wakiwapo WAFANYAKAZI WATUKUFU?
Mbona toka aseme anawajua wanaolipa wamtukanao Rais sasa kujipendekeza kwake kumekuwa kukubwa kama kuogopa wasitajwe?
WADUDU NDIO UBUNIFU WA MAKONDA?!

View: https://youtu.be/aFZXjQc901U?si=08otvhLulbWRB6VL

Ngoja tuone
 
Naona nyota ya Paul Makonda inang'aa sana jijini Arusha. Inaonekana wakazi wengine sana wa Arusha wamemkubali, Kihistoria Arusha haina kabila, nahisi huyu jamaa anaweza chukua Jimbo.
Hahahah, Mkuu em amka hii ndoto ni mbaya.

Nani kakwambia Arusha haina kabila?. Unataka wamuimbe Paulo kama Yahaya Mkuu?
 
Naona nyota ya Paul Makonda inang'aa sana jijini Arusha. Inaonekana wakazi wengi sana wa Arusha wamemkubali, Kihistoria Arusha haina kabila, nahisi huyu jamaa anaweza chukua Jimbo.
Yaani kila mahali ni chawa tu!
 
Kwani mada ni nini?Makonda alikemea ulevi kupromotiwa kwenye suala la Liquid!
Ulitaka azungumzie jambo lisilokuwa muafaka kwenye hiyo mada?
Shule mlikwenda kufanya nini?
Katika ile clip makonda hakukemea kupromotiwa ulevi pekee, na ndio maana alimtaja mpaka Dr shika, rudi uiskilize vzuri. Alichokemea yy ni kuwapromote vijana wa hovyo,
Kwa kifupi WAHUNI, ndo ambao alikemea kupromotiwa na kufanywa brand.

Sasa wadudu sio WAHUNI !? Kuna tofauti gani kati ya pierre na wadudu kwenye suala la uhuni ?

Ukisema kwa sababu pierre alikuwa alikuwa mlevi , na vp kuhusu Dr shika ambaye pia alimtaja !?

View: https://youtu.be/6u0BREZxKKo?si=kpn_0gc31GD1yjp5
 
Naona nyota ya Paul Makonda inang'aa sana jijini Arusha. Inaonekana wakazi wengi sana wa Arusha wamemkubali, Kihistoria Arusha haina kabila, nahisi huyu jamaa anaweza chukua Jimbo.
Ukiulizwa una miaka mingapi tangu uzaliwe utaona umedharaulika?Jitahidi uwe unatulia na unanyamaza ili tusijue kilema chako aisee!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katika sherehe za leo zinazoendelea mkoani Arusha na kwa nanmna zilivyofaana na kupendeza na kuvutia na kubwa zaidi kwa namna watu walivyofurika na kumiminika ni haijawahi kutokea katika Historia ya sherehe za Mei Mosi. Hii inabaki katika kumbukumbu ya Mei Mosi iliyohudhuriwa na watu wengi sana kuwahi kutokea katika Taifa letu.

Makonda ni Mwamba na bingwa wa mikakati na Jabali la mipango na hamasa. Jamaa anakubalika na kiongozi mwenye nyota kali sana ya kupendwa na watu pamoja na kuheshimika.leo Arusha imeitikia,kanda ya kaskazini imeamka na kwenda kuungana na Mwamba Makonda katika mapokezi mazito ya ugeni wa kitaifa na watu kutoka maeneo mbalimbali ya Taifa letu.

Kwa hakika ukitaka shuguli yako ipendeze katika jambo lolote lile ,basi wewe mkabidhi kazi hiyo Mwamba Makonda halafu muachie akufanyie kazi.kwa hakika leo Mwamba ameonyesha yeye ni mtu na nusu,ni kipenzi cha wana Arusha na watanzania wote kwa ujumla ,ni kipenzi cha vijana na watu wa makundi mbalimbali na ni kiongozi wa kutumainiwa na kutegemewa kwa Taifa letu.

Ipo siku Mwamba atashika nafasi za juu kabisa za uongozi ndani ya serikali yetu.ipo siku watu wataandamana na kumbeba Mwamba Makonda Mabegani mwao kumshukuru ,kumpongeza na kumtia moyo kwa uchapa kazi wake. Ukimchukia Mwamba Makonda unajiumiza tu maana kwa kadri unavyomchukia ndivyo anavyodhidi kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania. Usishindane na aliyepewa kibali na Mungu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Sawa!! Asante kwa taarifa nzuri!!
 
Mwamba Makonda anawatesa sana wapinzani na nyumbu wa CHADEMA. Mafuriko yaliyomiminika leo uwanjani mpaka wengine kukosa nafasi na kuamua kubakia nje ya uwanja kumewaumiza na kuwatetemesha sana sana CHADEMA, mpaka sasa wamebaki wanaweweseka tu kama wagonjwa wa malaria kali. Hapo bado Mwamba hajamaliza hata nusu mwaka.aa

Mwamba Makonda anawatesa sana wapinzani na nyumbu wa CHADEMA. Mafuriko yaliyomiminika leo uwanjani mpaka wengine kukosa nafasi na kuamua kubakia nje ya uwanja kumewaumiza na kuwatetemesha sana sana CHADEMA, mpaka sasa wamebaki wanaweweseka tu kama wagonjwa wa malaria kali. Hapo bado Mwamba hajamaliza hata nusu mwaka.
kwenye hili la mei mosi vichwa vyetu vikiwa na uwezo wa chini kidogo katika kufikiri basi ni vizuri humu ndani ya nchi tukaiona mei mosi katika kuitizama kwa mtizamo wa Kitaifa zaidi badala ya kuipa mtizamo wa itikadi za kichama ama kidini/kikabila.

zaidi tuione kwamba ni adhimisho la kilimwengu maana hata lilishaondokana kuwa la kitaifa na sasa ni la kidunia zaidi ndiyo maana linaadhimishwa ulimwenguni kote kwenye hiyo tarehe husika

sidhani kama mkuu wa mkoa alikuwa na maana yeyote ya kuwatenga ama kushindana na itikadi za kichama kwenye hili zaidi ni kwamba mpango wake ulikuwa ni kuwashirikisha woote bila kujali itikadi zao za kichama maana wafanyakazi kwenye mawneo yao ya kazi hawabaguliwa kiitikadi na hata mishahara na maslahi yao ya kazi hayajatofautishwa kiitikadi za kichama wala dini.

hongera serikali Kitaifa na serikali mkoa wa Arusha chini ya Makonda kwa kufanikisha kwa ufanisi sherehe za leo mei mosi 2024 na hongera sana kwa washiriki wote.
 
Hakika hiki ni kichekesho! Katika siku muhimu kama Mei Mosi kwa wafanyakazi.wanaowazia hatima ya kazi zao, mishahara na mafao yao ya kustaafu, pension zao, kupandishwa vyeo na kila linalowasibu eti ndio haya tena ya Makonda?
Mbele ya makamu wa Rais anayemwakilisha Rais mnasema bila aibu kuwa Makonda ni mbunifu kisa WADUDU?
Yaani bila aibu mnaleta vijana wakuwapeleka Rehab mbele ya Rais, mabalozi na wakuu wengine wakiwapo WAFANYAKAZI WATUKUFU?
Mbona toka aseme anawajua wanaolipa wamtukanao Rais sasa kujipendekeza kwake kumekuwa kukubwa kama kuogopa wasitajwe?
WADUDU NDIO UBUNIFU WA MAKONDA?!

View: https://youtu.be/aFZXjQc901U?si=08otvhLulbWRB6VL

Si mnapenda maigizo na mambo ya kipunguani,furahieni Sasa ndio hamasa zenyewe ambazo wanyonge wanazipenda,hata Jiwe alikuwa anakula eti mahindi aliyonunua Kwa wanyonge(wauza madafu) mnachekelea huku umaskini ukizidi kuwapausha 😁😁
 
Naona mmepaniki kwelikweli CHADEMA na kuumia sana baada ya kuona ngome zenu zinaendelea kusambaratishwa na kubomolewa na Mwamba Mwenyewe Makonda.
hiyo silaha amekuja nayo lisu ni ya kupiga kwenye mshono, hata ndugu zako wachuna ngozi kule mbozi wanapenda kusikia hiyo hoja ya Tanganyika.
 
Naona nyota ya Paul Makonda inang'aa sana jijini Arusha. Inaonekana wakazi wengi sana wa Arusha wamemkubali, Kihistoria Arusha haina kabila, nahisi huyu jamaa anaweza chukua Jimbo.

Walisema anakubaliki sana Dar. Pamoja na mbwembwe zote, alishindwa kuvuka hata hatua ya kura za maoni.

Mshauri agombee Arusha ili aweke historia ya kushindwa kupitishwa kwenye kura za maoni kwa mara ya pili mfululizo.
 
Naona nyota ya Paul Makonda inang'aa sana jijini Arusha. Inaonekana wakazi wengi sana wa Arusha wamemkubali, Kihistoria Arusha haina kabila, nahisi huyu jamaa anaweza chukua Jimbo.
Hata ujumbe wa nyumba kumi,wajumbe wenzie tunakula kichwaaaa🤪
 
Naona nyota ya Paul Makonda inang'aa sana jijini Arusha. Inaonekana wakazi wengi sana wa Arusha wamemkubali, Kihistoria Arusha haina kabila, nahisi huyu jamaa anaweza chukua Jimbo.
Aliekwambia Arusha hamna kabila ni nani?? Wenyeji wa Arusha ni wamasai na WA meru, hao unaona wanajiita waarusha wote ni Masai hao
 
Kwamba ubunge una maslahi kuliko u RC wa jiji la Arusha au dar maana makonda hata akiletwa dar bado UNYAMA.
 
Back
Top Bottom