KAZI ANAZOFANYA MH PAUL MAKONDA NDIO KAZI ZA KIONGOZI
Na
Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
Mimi ni shabiki mkuu wa aina ya siasa za watu kama Paul Makonda. nimekuwa nikimshabikia bila woga akiwa kwenye madaraka na alipokuwa nje ya uwanja wa siasa za kitaifa,
Nasikitika sana kusema watu wengi hawajui kuchagua zuri na baya, nimewahi kusikia kelele za wajinga wanaomchukia Mh Paul Makonda mimi huwa nacheka kwa kicheko cha Magufuli RIP. Paul Makonda ni kiongozi kinara katika muongo mzima tangu 2010's katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara, labla tunaweza kumweka kundi moja na Malema wa South Africa. katika siasa za kuwsinua wananchi, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni Paul Makonda ni Jembe tena sio la mkono, ni jembe la kitu zaidi ya trekta.
Tumekuwa na wimbi la vijana wamejikita kwenye siasa za kusambaza sambaza posters na habari na kwa bahati mbaya muda mwingine ndio wanaopewa nafasi kwa sababu tu wana maneno ya asali asali kwa viongozi, Paul Makonda sijawahi kumwona hivyo,
Paul Makonda ni kiongozi anayeingia field na kuwagusa kabisa wale wenye shida na haogopi kitu, mimi nikimsikiliza makonda najisikia raha sana kujua kumbe aina ya siasa za hivi inawezekana, yaani ukipewa kazi ni kufanya kazi sio kwenda kuwabembeleza watu na kuwalamba lamba miguu ili upate mali za wizi.
Nina mengi ya kusema kuhusu kiongozi huyu Jasiri, Mbunifu, Asiye na Chuki wala upendeleo, Muwazi, Asiyependa Majungu na Unafiki, PAUL MAKONDA.
SABAYA ARUDI KWENYE HATAMU KAZI ZIFANYIKE.
Ndimi
Comrade Ally Maftah
JITU LA MIRABA
CCM LIA LIA
MTIA NIA MCHACHACHALI JIMBO LA KAWE
View attachment 2987391View attachment 2987392