Sikujua kama hauna akili kiasi hicho, pole, hoja yangu kule mwanzo nilisema hivi, alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alifanya maigizo kama hayo, na nikatolea mifano kama ishu ya walimu kupanda daladala, ishu ya wamama waliotelekezewa watoto, hadi ishu ya madawa ya kulevya, ni ipi kati ya hizo ambayo iliacha alama lets say aliwafungulia labda wale akina mama waliotelekezewa watoto miradi fulani inayowaendeshea maisha hadi leo, au wale walimu alipendekeza itungwe hata sheria wawe wanapanda daladala bure hadi leo au ishu ya kuwataja wauza dawa za kulevya kwamba kuna watu kumi au ishirini walikamatwa, wakashtakiwa wakafungwa kwa juhudi zake, lakini hakuna hata kimoja kilichofanyika kiuendelevu zaidi ya kudhalilisha akinamama wa watu kwa lengo lake la kisiasa na kuwadhalilisha walimu pia na wanasiasa. Sana sana kwa kutafuta kiki alijifanya kuagiza fenicha kwa mgongo wa walimu kumbe alikuwa ana lengo la kupiga dili aje auze makontena kibao ya fenicha hizo, ila serikali tena chini ya Mwamba Magufuli ikamshtukia na ndiyo maana hata alipoenda kugombea ubunge akapigwa chini mazima.