Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Wanabuni tatizo kisha hao kurupu kwenye kulitatua.
Kuhusu kuanza kwa treni ya kisasa ya SGR, Makonda amesema kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichoketi Unguja hivi karibuni kiliwaita Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kutoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa.
"Tuliwahoji mbona kumekuwa mabadiliko ya kuanza kwa treni ya kisasa?
"Mwaka huu kama kuna ahadi nyingine zaidi ya kuiona treni ikitoka Dar es Salaam hadi Dodoma, wakatupa tena ahadi, CCM itakula kichwa, muda wa ahadi umekwisha," alisema.
Makonda ameeeleza hayo leo Ijumaa Januari 19, 2024 akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Bunju akiwa njiani kuelekea Bagamoyo mkoani Pwani.
Katibu huyo wa uenezi leo ameanza ziara ya mikoa 20 iliyopewa jina la "back 2 back".
CCM ina laana