Paul Makonda: Wanaotetea watoto wanaopata mimba shuleni wana akili za kuvaa nguo tu

Paul Makonda: Wanaotetea watoto wanaopata mimba shuleni wana akili za kuvaa nguo tu

Tatizo lake na la viongozi wengi hasa awamu hii ni uelewa na ushabiki/kujipendekeza. Hawana juhudi za kusoma tafiti wala kujielimisha katika mambo ya msingi. Wanaopata mimba wakiwa shuleni wengi wao ni watoto yaani under-18. Wengi wao wanasukumwa na umasikini wa familia zao au wanabakwa. Kuwatoa kwenye mzingo wa lindi la umaskini panahitajika juhudi za kuhakikisha wanapata elimu na kufikia ndoto zao. Ni haki yao ya msingi. Kwa kuwabagua au kuwatenga haiwasaidii wao wala vizazi vyao. Taratibu taifa linazidi kudidimia.
Mkuu unahangaika bure hayawezi kukuelewa haya madudu,Bashite ni zero brain
 
Ni kweli kabisa!

Sababu kubwa ni ukosefu wa mabweni kwenye Shule .

Wanafunzi wanalazimika kutembea mwendo mrefu sana wakati wa kwenda na kurudi shuleni.

Usafiri hakuna.

Wazazi/walezi hawana uwezo wa kumfikisha mtoto Shule kwa usafiri wa familia.

Usafiri wa umma hakuna.

Watoto wakike wanapokuwa njiani wakati wa kwenda au wakati wa kurudi hulazimika kuingia ushawishi wa ngono kupitia lifti za waendesha pikipiki na hatimae kupata mimba kama si magonjwa.

Wanafunzi wa kiume wengi huamua kuacha masomo njiani akiwa form 1 au 2 wengi huamua kuacha masomo sababu ya tabu wanayoipata kwenda mwendo mrefu kwa miguu kwenda shuleni na kushinda na njaa [emoji108][emoji108][emoji108]




Sent using Jamii Forums mobile app
TANZANIA HAKUNA ELIMU BURE.... ZAIDI YA KIZINGU MKUTI. ELIMU BURE NI JANGA LA TAIFA
 
lengo ni kuwafanya waseme NO kwa wazee wenye tamaa kama nyinyi [emoji3][emoji3]
Kwa taarifa yake na pia nafikri pia anajua na anamifano hai kama si kutokana na uongozi wake basi kwenye mapito ya maisha! Wako wasichana wengi ambao wamepata mimba na wakarudi shule baada ya kujifungua sasa hivi wanawasomesha watoto wao na wanamaisha mazuri. Na wapo kama wanavyotaka wao hawakuweza kurudi shule lakini sasa hivi na single mothers wanahangaika na maisha.

Lengo la kuwakataza hao watoto ni nini? labda wametenda dhambi sasa adhabu ndio hiyo ya kuwanyima elimu? Ok, Mwisho wa siku unajenga taifa la wasomi au la wajinga? taifa la omba omba au la kujitegemea? Kuteleza siyo kuanguka waachani watoto wenye nafasi waendelee na shule mwisho wa siku wakajitegemee badala ya kuwa omba omba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilani yao ya CCM mbona inasema mtoto wa kike akishajifungua watahakikisha wanarudi kusoma kama kawaida.Sasa RC yupo ACT au CHAdema
 
Inakuwaje mtoto wa shule anapachikwa mimba wakati mimi nimejaribu for.years na ilishindikana kutia goli? Najiuliza tu kimya kimya!
 
Back
Top Bottom