Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukuru Rais Samia kumteua mkuu wa mkoa wa Arusha kuongoza wananchi wenye akili nyingi na wapambanaji wasiokata tamaa na wanaojua hatma ya nchi. Ameyasema hayo kwenye kumbukizi ya waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika mjini Arusha.
Makonda amesema mji huo ni wa wajanja wanaoweza kutoka na kwenda popote kupambana na kujenga uchumi. Makonda amesema watu wa mkoa huo wametambulisha umahiri wao katika utafutaji ilhali kuna baadhi ya mikoa waganga wa kienyeji ni wengi lakini si kwa mkoa wa Arusha.
Kwenye hatua nyingine, Makonda amesema jiji la Arusha litafungwa camera na kuhakikisha taa zinawaka na kuwa na polisi wa kitalii watakaokuwa wanaendesha baiskeli kuhakikisha ulinzi umeimarika.
Makonda: Ifike hatua watu wakija jiji la Arusha wajisikie raha na kupiga picha na polisi wao ambao ndio wanaimarisha ulinzi katika jiji la Arusha.
Pia tumekubaliana kuondoa mabango yote yanayochafua sura ya jiji la Arusha na kuhakikisha tunakuwa na muonekano mzuri ili watalii watakapokuja wasione kama watu tusioweza kujipanga, tunatembelea miji yao tunaona namna ilivyo.
Pia Makonda amemuomba Rais Samia kilomita 20 za barabara za lami kwani katika ya mji wa Arusha kuna barabaraba mbovu, amedai kuwa wananchi wa mkoa huo wamemtuma akamuombe 'mama yake' barabara na wanampima kama ni mama yake kweli.
PIA, SOMA:
Uteuzi wa Ukuu wa Mkoa Arusha
Matukio baada ya Uteuzi
Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine